Polisi wamzuilia mwanamke kwa madai ya mauaji Machakos

Anayedaiwa kutekeleza mauaji ya mumewe baada ya ukosefu wa maelewano baina yake na mumewe

Muhtasari

• Mshukiwa anadaiwa kutekeleza mauaji hayo baada ya ugomvi wa kinyumbani na mumewe.

• Mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Matuu ukisubiria upasuaji huku polisi wakiendelea na uchunguzi

crime scene
crime scene

Polisi katika eneo la Matuu kaunti ya Machakos wanamzuilia mwanamke wa umri wa miaka 21 kwa madai ya kumuua mumewe kwa kumdunga kwa kisu siku ya Jumatano.

Mshukiwa alikamatwa baada ya kupokea huduma za matibabu katika hospitali ya Matuu alikotibiwa majeraha aliyodai alijidunga kutokana na hasira.

Kulingana na majirani, walisema kuwa walisikia nduru kutoka kwa nyumba ya wanandoa wale na walipofika kufahamu kilichokuwa kinajiri, walimpata mshukiwa akiwa amemshikilia mume wake kwa jina Rodney Muasia wa miaka 23.

Aidha majirani pia walisema mshukiwa aliwaeza kuwa mumewe alikuwa amemkosea ndiposa akamdunga kwa kisu cha jikoni.

Polisi walifanikiwa kupata kisu kilichotumika kikiwa na damu na kitatumika kama ushahidi dhidinya mshukiwa katika mahakama.

Hata hivyo, polisi walisema kuwa mshukiwa atafanyiwa vipimo vya afya ya akili katika harakati ya uchunguzi wa kisa hicho cha mauaji.

Mwili wa mwenda zake ulipelekwa katika mochwari  ya hospitali ya Matuu ukisubiria kufanyiwa upasuaji huku maafisa wa usalama wakiendeleza uchunguzi.