Bei ya mafuta yaongezeka kwa shillingi 3.40

Bei mpya zilianza kutumika saa sita usiku wa kuamkia Jumatatu, Mei 14 hadi saa sita usiku wa Juni 14, 2023.

Muhtasari

•Ongezeko hili linamaanisha bei ya petroli imeongezeka hadi shilingi 182.70, ile ya dizeli ikipanda hadi 168.40 na mafuta taa yatauzwa kwa shilingi 161.13 jijini Nairobi.

Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli nchini (EPRA) imetangaza kuongeza bei ya  mafuta nchini.

Katika mabadiliko hayo, bidhaa hio mihimu imeongezeka kwa shilingi 3.40 kwa lita ya petroli, shillingi 6.40 kwa mafuta ya dizeli na shillingi 15.19 kwa lita moja ya mafuta ya taa.

Ongezeko hili linamaanisha bei ya petroli imeongezeka hadi shilingi 182.70, ile ya dizeli ikipanda hadi 168.40 na mafuta taa yatauzwa kwa shilingi 161.13 jijini Nairobi.

“Kwa mujibu wa Kifungu cha 101(y) cha Sheria ya Petroli ya 2019 na Notisi ya Kisheria Na.192 ya 2022,EPRA imepania kubadilisha bei za juu zaidi za rejareja na za jumla za bidhaa za petroli ambazo zitaanza kutumika kuanzia tarehe 15Mei hadi tarehe 14 Juni 2023.” Taarifa hio ilisoma.

Bei hizo ni pamoja na asilimia 8 ya ushuru wa Ongezeko la Thamani ya bidhaa (VAT)

Katika taarifa kwenye vyombo vya Habari, mamlaka hiyo iliashiria ongezeko hilo ni baada ya kuzingatia uzani wa wastani wa gharama ya bidhaa za petroli iliyosafishwa kutoka nchi za nje.

Bei mpya zilianza kutumika saa sita usiku wa kuamkia Jumatatu, Mei 14 hadi saa sita usiku wa Juni 14, 2023.