KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Migori na Kirinyaga.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu ya mtaa wa Kitsuru ikiwa ni pamoja na Gachie, Kirawa Rd, Ngecha Rd, Nyari South Estate na New Muthaiga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na kumi na moja jioni.
Sehemu ya mtaa wa Dandora ikiwa ni pamoja na Total Petrol Station, Sakina Gas na viunga vyake pia haitakuwa na stima katika kipindi hicho.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Kawaida na Hospitali ya Nazareth katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Migori, sehemu za maeneo ya Kehancha na Ntimaru zitapoteza nguvu za umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri. Sehemu zitakazoathirika ni pamoja na Uwanja wa ndege wa Migori, KEFRI, Nyanchabo, Masaba, Nyamamagagana, Kurutyange, Ikerege, Tarawiti, Koego, Nyametaburo, Nyamaranya, Karosi, Mji wa Kehancha, St. Kizito, Maeta, Kegonga, Igena, Nyabikongori, Kebarisia, Mosweto, Nyamutiro, Kebaroti, Makararangwe na Ntimaru.
Maeneo ya Mutitu na Ematex katika kaunti ya Embu pia yataathirika na ukosefu wa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.