Fahamu maeneo ya Kenya yatakayoathirika na kukatizwa kwa stima Jumanne - KPLC

KPLC imetangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme Jumanne mchana.

Muhtasari

•Kaunti za Kenya ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni, Kajiado, Migori, Homa Bay,Nyeri, Embu, Mombasa na Kilifi.

•Katika kaunti ya Nairobi, sehemu ya maeneo ya Riverside Drive na Tende Drive yataathirika na kukatizwa kwa umeme Jumanne mchana.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Januari 16.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme Jumanne mchana.

Kaunti za Kenya ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni, Kajiado, Migori, Homa Bay,Nyeri, Embu, Mombasa na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu ya maeneo ya Riverside Drive na Tende Drive yataathirika na kukatizwa kwa umeme Jumanne mchana.

Sehemu ya eneo la Kalimoni katika kaunti ya Machakos pia itakosa umeme siku ya Jumanne.

Katika kaunti ya Kajiado, maeneo ambayo yatakosa umeme ni pamoja na Kitengela na Kibiko- Kimuka- Saikeri.

Maeneo ya Uriri, Bware na Kakrao katika kaunti ya Migori pia yatashudia kukatizwa kwa umeme siku ya Jumanne.

Katika kaunti ya Homa Bay, maeneo ya Mbita, Sindo na Nyadhiwa ndiyo yataathirika na kukatizwa kwa umeme.

Maeneo ya Kirichu na Kagumo High pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme siku ya Jumanne mchana.

Sehemu za maeneo ya Mayori, Mariari, Kiambere na Gacabari katika kaunti ya Embu pia zitakosa umeme.

Katika kaunti ya Mombasa, sehemu za maeneo ya Nyali, VOK na Bombolulu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Eneo la Bofa katika kaunti ya Kilifi pia itaathirika na kukatizwa kwa umeme Jumanne mchana.