USALAMA WA KITAIFA

Kindiki - Bunduki zote zinazomilikiwa na raia kiharamu lazima zipatikane

″Idara ya usalama itaendelea na oparesheni hadi wawafurushe majambani wote kutoka majifichoni,″ alisema.

Muhtasari

•Kaunti za Mandera,Baringo,Turkana na Marsabit ni miongoni mwa kaunti ambazo zimekumbwa na ukosefu wa usalama kutokana na uvamizi wa mara kwa mara wa majambazi wanaoiba mifugo.

•Waziri wa usalama wa kiataifa  na masuala ya ndani Prof. Kithure Kindiki ametua kaskazini mwa nchi kaunti ya Mandera hivi leo. Nia yake ikiwa ni harakati za kuimarisha usalama  maeneo hayo. na kaunti zinazozingirwa na bonde la ufa kaskazini.

Waziri wa usalama wa kiataifa  na masuala ya ndani Prof. Kithure Kindiki ametua kaskazini mwa nchi, katika kaunti ya Mandera hivi leo. Nia yake ikiwa ni harakati za kuimarisha usalama katika eneo hilo na kaunti zinazozingirwa na bonde la ufa kaskazini.

Kaunti za Mandera,Baringo,Turkana na Marsabit ni miongoni mwa kaunti ambazo zimekumbwa na ukosefu wa usalama kutokana na uvamizi wa mara kwa mara wa majambazi wanaoiba mifugo.

″Bunduki zote zinazomilikiwa na raia kiharamu lazima zipatikane.Mashirika ya usalama yamejihami kukabiliana na majambazi wa wizi wa mifugo katika eneo la  kaskazini mwa Bonde la Ufa.″ Kindiki alisema.

Aliendelea kuwapongeza wakaazi wa kaunti ya Samburu, kwa kuwasilisha bunduki 96 na risasi zaidi ya mia wiki chache zilizopita.

Kindiki aliendelea kusema kwamba, serikali itaendelea kushirikiana na wakaazi wa Samburu kuwavumbua majambazi na kuwapokonya silaha.

″Idara ya usalama itaendelea na oparesheni hadi wawafurushe majambani wote kutoka majifichoni.″