Tazama maeneo ambayo hayatakuwa na stima leo, Jumatano - KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Januari 17.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. 

•Sehemu za maeneo ya Greatwall 1&2 apartments na Sabaki katika kaunti ya Machakos zitakosa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.

Kenya Power

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Januari 17.

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Kiambu, Machakos, Kajiado, Nakuru, Bomet, Busia, Migori, Embu na Nyeri.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu za maeneo ya Clavers Hotel na TIBS zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Greatwall 1&2 apartments na Sabaki katika kaunti ya Machakos zitakosa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.

Sehemu ya mji wa Kajiado katika kaunti ya Kajiado pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Nakuru, sehemu za maeneo ya Free Area, Kisulsuli, Sec 58, Bedi na Central Bank zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Siongiroi, Olbutyo Chebunyo, Emarti na Kaboson katika kaunti ya Bomet yatakosa umeme kati ya saa tatu na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Busia, baadhi ya sehemu za maeneo ya kijiji cha Maseno, Korinda na kampuni ya sukari ya Olepito yataathirika na kukatizwa kwa umeme.

Katika kaunti ya Migori, maeneo ya Kowino, Nyabohanse na Isibania ndiyo yatakayoathirika.

Sehemu za maeneo ya Kirima, Munyori, Kamunyange na Kiametho katika kaunti ya Embu pia yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Nyeri, sehemu za maeneo ya Chaka Brookside na Goldmine Clasher ndiyo yataathirika na kukatizwa kwa umeme.