logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aende au amuoe 'sidechick wake'-Mke asukumia mume mhanyaji Kipusa

Lakini je kwa nini umtafute mpango wa kando kama huna uwezo.

image
na Radio Jambo

Habari29 March 2022 - 10:41

Muhtasari


  • Kitumbua kilizidi kuingi mchanga kwani Purity alishikilia msimamo wake kuwa kama mumewe hatamuoa mke mwingine haya basi hakutakuwa na amani nyumbani mwake
sad woman

Ni furaha ya kila mwanamke kuona mumewe akiwa naye pekee kama mpenzi pasi uhusiano wa kando.

Lakini mambo si kama hayo kwa Purity ambaye alisumia mumewe mhanyaji kipusa ambaye alikuwa ana kula mahaba naye.

Kauli yake Purity iliwashangaza wengi baada ya kumwaya mtama yale mumewe wake amekuwa akifanya gizzani au bila yake kujua.

“Usidhani sijui mambo unayoendeleza mtaani. Najua una mpango wa kando ndio maana huwa hautulii hapa nyumbani. Kama hautosheki na mimi nakusihi uoe mwanamke mwingine na sitakuwa na shida. Nitakubali kuwa na mkemwenza,” demu alimwambia jamaa.

Kitumbua kilizidi kuingi mchanga kwani Purity alishikilia msimamo wake kuwa kama mumewe hatamuoa mke mwingine haya basi hakutakuwa na amani nyumbani mwake.

Jamaa huyo alikana madai ya mkewe, huu akishikilia kwamba hana uwezo wa kuishi na wanawake wawili.

Lakini je kwa nini umtafute mpango wa kando kama huna uwezo.

Haya basi 'side chicks 'habari ni kwamba hamna mwanamume atamuacha mkewe kwa ajili yako.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved