Niliwapata mchana peupe-Mwanamke asimulia jinsi mama yake alivyomnyakua mpenzi wake

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi mama yake alivyomnyakua mpenzi wake

sad woman
sad woman

Tumekuwa tukiyaona kwenye filamu, na kupuuzilia mbali huku tukisema kwamba ni uigizaji tu na hamna mtu ambaye ana akili timamu anawea fanya mambo mengine.

Hata wazazi wakati huu na karne hii hawaheshimu ndoa za watoto wao, kwani wameona tu ni jambo la kawaida kuishi na watoto wao baada ya kufunga harusi.

Mwandadammoja aliwaacha wanamitandao midomo wazi baada ya kufichua kwamba mama yake alimnyakulia mpenzi wake miezi chache tu baada ya kufunga pingu za maisha na mpenziwe.

Huu hapa usimulizi wake;

"Kusema ukweli sijawahi ona kwamba nina mama, ndio amenilea na sijawahi jua baba yangu mzazi,ni jambo ambalo hakutaka kuniambia au tulizungumzie tukiwa sebuleni

Niliweza kufunga ndoa nikiwa na miaka 28, lakini sikujua kwamba mama yangu alikuwa tayari kwenye uhusiano na mume wangu

Siku moja niliwapata mchana peupe wakiwa kwenye mahaba tele, nilienda kazi na kurudi bila kuwataarifu, hapo ndipo nilikata uhusiano wangu na mama yangu na mume wangu, na sioni kama nitawahi msamehe mama yangu, kwa kumkubali mwanamume aliyekuwa na uhusiano naye kunioa

Hiyo ni laana, natamani ningemjua baba yangu mzazi."