'Hakimu anastahili tuzo,'Sonko ampongeza hakimu baada ya kufanya harambee kwa wanandoa walioshtakiwa kwa kuiba ngano

Muhtasari
  • Sonko ampongeza hakimu baada ya kufanya harambee kwa wanandoa walioshtakiwa kwa kuiba ngano
Image: MIKE SONKO/FACEBOOK

Aliyekuwa gavana wa Nairobi namwanaiaji ugavana kaunti ya Mombasa Mike Sonko kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook amemongeza hakimu aliyewafanyia harambee wanandoa walioshatakiwa kwa kuiba ngano.

Akizungumzia suala hili, Sonko amefichua kuwa atahakikisha anawasaidia kwenda bila malipo kutokana na ukweli kwamba mshukiwa alidaiwa kukiri alichofanya.

Huku akitoa taarifa fupi ya kile kilichotokea, katika mahakama hiyo ya Mombasa Sonko aliandika ujumbe unaosoma;

"Hakimu huyu anastahili tuzo 1.) Hakimu mkuu wa Mombasa Vincent Adet aliamuru Harambee ndogo kuchangisha pesa kwa mwanamke wa makamo ambaye alishtakiwa pamoja na mumewe kwa kuiba kilo moja ya unga wa ngano. 2.) Ali pamoja na mumewe Evans Odhiambo walikuwa wameshtakiwa kwa wizi kinyume na kifungu cha 268 (1) kama kilivyosomwa na kifungu cha 275 cha kanuni ya adhabu. 3.)

"Kwa misingi ya kibinadamu, hasa kwa mshitakiwa wa kwanza, nimezingatia mazingira ambayo kosa lilifanyika na ninasikitikia hali yake, akiwa na watoto watatu chini ya uangalizi wake na hakuna chanzo cha mapato na nina maoni kwamba wacha tumnunulie kilo cha unga wa ngano na nyama kwa leo."

Vile vile, Sonko amefichua kuwa atatafuta njia ambazo Vijana wa Kenya wanaweza kuajiriwa ili kupunguza visa vya uhalifu vinavyoongezeka nchini ambavyo kulingana naye, vimesababishwa na kuongezeka kwa idadi ya Wakenya ambao hawana. ajira licha ya kwamba wana ujuzi wa kutosha.