logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatajiondoa kwenye kinyang'anyiro-Diana Marua amtetea mumewe

Hii sio mara ya kwanza azma ya msanii huyo kukumbwa na matatizo.

image
na Radio Jambo

Habari28 June 2022 - 12:00

Muhtasari


  • Mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati ambaye pia analenga kiti cha ubunge Mathare kupitia tikiti ya Jubilee amemkosoa vikali katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna
Diana Marua

Mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati ambaye pia analenga kiti cha ubunge Mathare kupitia tikiti ya Jubilee amemkosoa vikali katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna kwa matamshi yake kwamba vuguvugu la Azimio lacUmoja limeamua kumuunga mkono Anthony Oluoch wa ODM katika kinyang’anyiro cha ubunge Mathare.

Hata baada ya maamuzi ya Sifuna Bahati akihutubia wanahabari siku ya Jumatatu alisema kwamba hatajiuzulu kwa ajilo ya mtu yeyote.

Bahati ambaye alichukizwa na matakwa hayo ya katibu mkuu wa ODM aliamua kukunja shati na kujibwaga ulingoni katika kutupiana maneno makali na Sifuna huku akimtaka aachane na eneo bunge la Mathare kabisa kama kweli anataka kura za eneo bunge hilo kumvusha kuwa Seneta wa Nairobi.

Mimi nashangaa na huyu Sifuna, 2013 alikuwa na tikiti ya ODM huko Kanduyi na akaanguka, 2017 alikuwa na tikiti ya ODM na bado akaanguka Seneta hapa Nairobi. Na huyu jamaa vile anaendelea kuchezea youth, hana heshima kwa youth, hata huu mwaka tutakuwa tulifanya maamuzi mabaya kama Azimio, ataanguka tena! Sifuna fagia kwako."

Huku mkewe Bahati akimtetea, aliweka mambo wazi kuwa Bahati hatajiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa ajili ya mtu yeyote.

"Kelvin Bahati mbunge wa Matahre ajaye, hatajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kwa ajili ya mtu yeyote PERIOD," Aliandika Diana.

Hii sio mara ya kwanza azma ya msanii huyo kukumbwa na matatizo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved