Alinifunga sehemu zangu za siri kabla ya kuaga dunia-Mwanamke asimulia masaibu haya

Nikiwa kwenye ziara zangu, katika kijiji kimoja, nilikutana na mwanamke ambaye alinisimulia kile ambacho mumewe mchawi alimfanyia miaka iliyopita.

Muhtasari
  • Ni vitendo ambavyo tumekuwa tukiskia na kuviona kwenye televisheni, huku vitendo vingi vikiwashangaza wengi
  • Ndio wengi wanasema kuwa ni nyakati za mwisho, kwani mambo ambayo yanatendeka sio ya kawaida
sad woman
sad woman

Ni vitendo ambavyo tumekuwa tukiskia na kuviona kwenye televisheni, huku vitendo vingi vikiwashangaza wengi.

Ndio wengi wanasema kuwa ni nyakati za mwisho, kwani mambo ambayo yanatendeka sio ya kawaida.

Nikiwa kwenye ziara zangu, katika kijiji kimoja, nilikutana na mwanamke ambaye alinisimulia kile ambacho mumewe mchawi alimfanyia miaka iliyopita.

Kulingana na Regina, mumewe alimfunga sehemu zake za siri kabla ya kuaga dunia ili asiweze kufanya ngono au kuoleka na mwanamume mwingine.

"Mume wangu alikuwa mchawi hatari humu kijijini kabla ya kuaga dunia mwaka wa 2002,singeweza enda nje ya ndoa kwani alifahamu vizuri jinsi ya kunifunga endapo nitafanya tendo la ndoa na mwanamume mwingine

Hata baada ya kufariki, nilijaribu kufanya tendo la ndoa na mwanamume mwingine lakini nilichokiona na kushuhudia kilinikomesha, baada ya kufanya tendo la ndoa na mwanamume huyu,sehemu zangu za siri zilianza kufura na kuwa na vidonda hadi pale nilienda kwa mchawi mwenzake na kunitoa aliyoyafanya mume wangu

Kwa hivyo tuseme kuwa alinifunga milele, ili niwe wake ata akiwa ameaga dunia, maisha hayajakuwa rahisi kwangu,kama mjane.

Regina alifanikiwa pale alipopatana na mtumishi wa Mungu na kumuombea na kumwondolea madhara yote ambayo mumewe alikuwa amemfunga nayo.

"Ndio namshukuru Mungu kwani ameniponya lakini wakati wangu wa kufunga ndoa tena umepita kwani nina wajukuu, lakini namshukuru Mola kwa yote na uhai, sio lazima niweze kuolewa tena lakini ni matamanio ya kila mwanamke kuwa na mpenzi au mume."