logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sikuwahi kufukuza mtu yeyote kutoka kwa serikali - Uhuru

Akizungumza Jumapili jioni, mkuu huyo wa nchi alisema hakuwahi kumfukuza mtu yeyote

image
na Radio Jambo

Habari07 August 2022 - 18:02

Muhtasari


  • Akizungumza Jumapili jioni, mkuu huyo wa nchi alisema hakuwahi kumfukuza mtu yeyote kutoka serikalini
Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta amekanusha madai kwamba aliwafukuza baadhi ya waliokuwa washirika wake kutoka kwa serikali.

Akizungumza Jumapili jioni, mkuu huyo wa nchi alisema hakuwahi kumfukuza mtu yeyote kutoka serikalini.

"Hata wale waliosema handshake ilibadilisha mambo serikalini. Je, kuna mtu yeyote niliyemfukuza kazini? Sijawahi kumfukuza mtu yeyote serikalini," Uhuru alisema.

Haya yanajiri kufuatia matamshi mbalimbali ya naibu wake na mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto akidai kuwa alifurushwa kutoka serikalini.

DP alisema awali jukumu lake lilikabidhiwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti na mratibu wa mipango na miradi ya maendeleo ya serikali.

Akizungumza Jumapili usiku na vyombo vya habari, Uhuru alisema mabadiliko pekee yatakuwa kwamba hatakuwa Rais tena na hatakuwa akifanya kazi kutoka Ikulu.

“Hatuendi popote, bado tutafanya kazi pamoja, kazi ni kubwa, nimebakiza kazi moja tu na nitaanza nyingine,” alisema. [07/08, 20:56] Gm na mabadiliko ya uzoefu.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved