Ngirici amjibu Waiguru baada ya madai ya wizi wa kura Kirinyaga

Waiguru pia alimshutumu Ngirici kwa kupeleka majambazi katika kituo cha kuhesabia kura cha Kianyaga

Muhtasari

Ngirici amjibu Waiguru baada ya madai ya wizi wa kura Kirinyaga

Mgombea ugavana wa Kirinyaga Wangui Ngirici amemjibu Gavana wa sasa Anne Waiguru kuhusu madai ya wizi wa kura.

"Mlango pekee wa nyuma ambao tunajua ulikuwa NYS wakati wa umiliki wako. TUPO SITE!" Ngirici alisema katika taarifa siku ya Jumatano.

Waiguru alidai kuwa masanduku mawili ya kura yaliingizwa  katika kituo cha kujumlisha kura cha Kianyaga wakati wa shughuli ya kuhesabu kura.

"Sanduku mbili za kura zilizo na kura ya magavana huingia Kirinyaga kupitia mlango wa nyuma mchana kweupe! LAZIMA ziondolewe na kujumlisha kura lazima kukomeshwa," gavana huyo aliandika.

Waiguru pia alimshutumu Ngirici kwa kupeleka majambazi katika kituo cha kuhesabia kura cha Kianyaga ili "kuvuruga uhesabuji kura."

Ngirici, ambaye anawania kama mgombeaji huru, Jumanne alisema ana imani na zoezi la upigaji kura.

Kujumlisha kura kwa sasa kunaendelea huku nchi ikisubiri kutangazwa rasmi kwa washindi kutoka kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.