logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais wa Zambia ampongeza rais mteule William Ruto

“Hongera Dkt William Samoei Ruto, kwa kutangazwa kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya #Kenya" - Hakainde Hachilema.

image
na Radio Jambo

Habari05 September 2022 - 11:59

Muhtasari


• "Tunatazamia kufanya kazi na Mheshimiwa @WilliamsRuto kuimarisha na kuimarisha uhusiano mzuri wa kihistoria kati ya Zambia na Kenya" - Hakainde

Rais wa Zambia amempongeza rais mteule William Ruto

Rais wa Zambia Hakainde Hachilema amekuwa kiongozi wa hivi punde kutuma pongezi zake kwa rais mteule William Ruto, dakika chache baada ya mahakama ya upeo kudumisha ushindi wake.

Hachilema ambaye aliingia kwenye historia kama mwanasiasa wa upinzani wa muda mrefu aliyewania mara kadhaa pasi na kushinda na akaja kushinda baadae alimtambua Ruto kama kiongozi shupavu ambaye ataweza kuendeleza uhusiano wao mzuri baina ya mataifa haya.

“Hongera Dkt William Samoei Ruto, kwa kutangazwa kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya #Kenya. Tunatazamia kufanya kazi na Mheshimiwa @WilliamsRuto kuimarisha na kuimarisha uhusiano mzuri wa kihistoria kati ya Zambia na Kenya kulingana na vipaumbele vyetu vilivyoshirikiwa kwa watu wetu wawili,” aliandika Hachilema kweney mtandao wake wa Twitter.

Hachilema ameingia kwenye orodha ya viongozi wengine wengi kutoka mataifa mbali mbali amabo wanaendelea kumimina pongezi zao kwa rais William Ruto.

Ruto aliibuka mshindi katika uchaguzi wa Agosti 9 ambapo alikuwa anajaribu bahati yake kwa mara ya kwanza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga ambaye alikuwa anajitupa uwanjani kwa mara ya tano mtawalia na kushindwa mikumbo yote.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved