Huwezi kutumia Cherera kupata bonga points kwa Ruto - Omanwa amzomea Balala

Omanwa ni mwandani wa Ruto na alimwambia Balala kukoma kutumia masuala fulani ili kumpendeza Ruto kumpa kazi

Muhtasari

• Jana waziri anayeondoka wa utalii Najib Balala alizungumza kwamba Cherera na makamishna wengine watatu walioasi IEBC sharti wachukuliwe hatua za kisheria.

Dennis Omanwa amzomea Balala vikali dhidi ya kujitafutia kazi kwa Ruto
Dennis Omanwa amzomea Balala vikali dhidi ya kujitafutia kazi kwa Ruto
Image: Facebook

Mwandani wa karibu wa rais William Ruto, Dennis Omanwa amemjia juu Waziri wa utalii anayeondoka Najib Balala kwa kuvunja kimya chake kuhusu makamishna wanne waasi wa IEBC waliojitenga na matokeo ya IEBC.

Makamishna hao wanaongozwa na naibu mwenyekiti wa IEBC, Juliana Cherera.

Baada ya kimya cha muda mrefu, jana Waziri Balala alivunja ukimya huo kwa kuweka wazi kwamab makamishna hao walikuwa nusra walitumbukize nchi katika mzozo wa kivita baada ya kujitenga na matokeo dakika ya mwisho kabisa mnamo Agosti 15 matokeo ya urais yalipokuwa yanatarajiwa kutangazwa.

Balala alisema makamishna hao ni sharti wawajibishwe kwa kitendo chao hicho cha kutaka kuiteketeza nchi na hawatasazwa hata kidogo.

“Ubinafsi wa kutokujali lazima ushughulikiwe vilivyo au utakuja kurudi kutuhukumu.watu ambao nusra wasababishe umwagikaji wa damu usiku ule IEBC ikitangaza matokeo, watu kama Cherera ni lazima wawajibishwe vilivyo. Si kulipa kisasi lakini ni kwa sababu ya matakwa ya wananchi,” Balala alinukuliwa akisema.

Matamshi haya yake japo yalipokelewa vizuri, kuna baadhi ya watu walihisi kwamba anajipendekeza kwa serikali mpya ili kupata kazi.

Mmoja wa watu hao ni mwandani wa Ruto, Dennis Omanwa ambaye amempasha Balala kwamba ameanza kujileta kwangu kwangu karibu na ubavu wa Ruto ili kupewa kazi ila akamuonya kwamba hawezi pat ahata chembe.

“Huwezi kutumia "Cherera" kupata alama nyingi za bonga katika serikali ya Rais Ruto. Wale wanne wa Opaque wana muziki wao wa kucheza ngoma,” Omwanwa alimzomea Balala kwa maneno makali ya kukata maini.