Idara ya mahakama yakanusha uvumi kuwa majaji Wanjala na Mwilu wamejiuzulu

Awali kulikuwep na uvumi mitandaoni kwamba jaji Smokin Wanjala na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu wamejiuzulu

Muhtasari

• Uvumi huo ulikuwa unasema kwamba majaji Smokin Wanjala na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu wametuma barua za kuomba kuachia ngazi kwa sababu zisizojulikana.

Idara ya mahakama yakanusha madai kwamab majaji wake baadhi wametuma ombi la kutaka kujiuzulu
Idara ya mahakama yakanusha madai kwamab majaji wake baadhi wametuma ombi la kutaka kujiuzulu
Image: maktaba

Wikendi iliyopita kulikuwa na uvumi uliokuwa unasambazwa mitandaoni kwamba baadhi ya majaji wa mahakama ya upeo na amabao walikuwa katika jopo la majaji saba kuamua kesi ya baada ya uchaguzi wa urais wamejiuzulu.

Uvumi huo ulikuwa unasema kwamba majaji Smokin Wanjala na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu wametuma barua za kuomba kuachia ngazi kwa sababu zisizojulikana.

Baada ya uvumi huo kusambaa pakubwa, wengi waliuhusisha na uamuzi wa kesi ambao ulisomwa na jaji mkuu Martha Koome kuidhinisha ushindi wa Ruto kama rais.

Kupitia ukurasa wa Twitter, idara ya mahakama imepuuzilia mbali taarifa hizo za kujiuzulu kwa majaji hao wawili ikizitaja kuwa za uongo na za kupotosha.

Wambea wenye midomo walikuwa wameanza kuzua kwamba kuzjiuzulu kwa wawili hao kulikuwa nip engine tofauti za kuelewana, huku wengine wakidai wawili hao huenda walikuwa katika upande wa kutaka ushindi wa Ruto kubatilishwa.

Ila kama kila mtu anavyojua, siku zote binadamu hakosi la kuamba, cha msingi ni kwamba mahakama imesema Wanjala na Mwilu bado ni majaji wa mahakama ya upeo ha madai ya wao kutoa barua za kutaka kujiuzulu ni uvumi usio na mashiko wala minato.

Wakenya bado wanazidi kuhesabu siku 21 tangu jopo hilo liidhinishe ushindi wa Ruto ambapo jaji mkuu Martha Koome aliahidi kutoa nakala ya uamuzi huo kwa ukamilifu ili kuonyesha ni kwa jinsi gani waliafikia uamuzi wa kutupilia mbali ombi la Azimio la kutaka ushindi wa rais mteule kubatilishwa.