Azimio wamtema Boniface Mwangi kutoka makundi yake ya WhatsApp

Mwangi alisema kuondolewa huku ni kutokana na waraka wake wa awali kusema sababu zilizofanya Raila kushindwa na Ruto

Muhtasari

• Awali Mwangi aliandika ujumbe mrf uakielezea sababu zilizofanya Ruto kuwachachafya katika kipute cha urais.

• "Kama ningetaka kuwaburuza na kuwataja watu mahususi waliotusababishia kushindwa" - Mwangi

Mwanaharakati Boniface mwangviateta kuondolewa whatsapp na azimio
Mwanaharakati Boniface mwangviateta kuondolewa whatsapp na azimio
Image: Facebook

Mwanaharakati Boniface Mwangi ameteta kuondolewa katika makundi yote ya mtandao wa WhatsApp ya muungano wa Azimio.

Kuondolewa kwake kunakuja saa chache tu baada ya mwangi kuandika waraka mrefu alisimulia jinsi Azimio walizembea katika kampeni zao na kupelekea kushindwa na mrengo wa William Ruto.

Mwangi ambaye alinyoosha mambo kwa kuweka wazi kwamab yeye hakupewa kazi na muungano wa Azimio kuwapigia debe bali alikuwa tu kaam mtu wa kujitolea kutokana na sababu nyingi alizozitaja kwamba Martha Karua ni rafiki yake mkubwa na ilikuwa ajitolee ili kumsaidia kusukuma ajenda za Azimio, ambako alikuwa kama mgombea mwenza wa urais.

Mwangi alisema sababu moja ya Azimio kupoteza ni uzembe na kujiamini kupita kiasi kwamab wameshinda huku wakiwadunisha wapinzani wao.

“Tulidhani ushindi ulikuwa wetu kwa sababu Rais Uhuru Kenyatta aliwaidhinisha na kuwafanyia kampeni Raila na Martha. Tulishindwa kufanya kazi kubwa ya kupanga mikakati, kuandaa na kuhamasisha msingi wetu kujitokeza kupiga kura, hasa katika ngome zetu. Tulishindwa kuwalinda mawakala wetu dhidi ya vishawishi vya rushwa kirahisi kutoka kwa wapinzani wetu,” Mwangi alisema.

Mwangi alizungumza pia kwamab ujasiri aliokuwa nao wakati kuhesabiwa kwa kura kunaendelea ni kutokana na simu waliyopigiwa na mmoja wa vigogo ndani ya Azimio akiwahakikishia kwamba washaramba urais.

“Sekretarieti hiyo ilipuuza maoni ya jinsi ya kufanya kampeni hiyo isikike kwa Wakenya ikiwa ni pamoja na: kuwaondoa wazee, na watu wanaokabiliwa na mashtaka ya uhalifu kwenye mikutano yetu na kupata sauti nyingi za vijana kwenye jukwaa la kampeni, na kuwa na uongozi wa mitaa katikati badala ya kuwa na mtu mmoja. endesha onyesho kwenye mikutano yote. Siasa ni za ndani. Azimio alishindwa kujipanga ndani. Tungefanya mikutano ya hadhara na kutoka mara moja na timu tuliyokuja nayo. Hakukuwa na mtu aliyebaki nyuma kuhakikisha kuwa ujumbe huo ulikuwa umekita mizizi,” Mwangi alifunguka katika waraka huo mrefu.

Baada ya kufunguka huku, Mwangi saa chache baadae alienda kwenye Twitter yake na kuteta kwamab Azimio wamemtoa kwenye makundi yote ya Whatsapp.

“Nimeondolewa kwenye vikundi vyote vya kampeni vya WhatsApp ambayo ni hatua ya kipumbavu na ndogo. Kama ningetaka kuwaburuza na kuwataja watu mahususi waliotusababishia kushindwa, ningefanya hivyo lakini sikufanya hivyo. Inaonekana mabadiliko yangu katika timu yamefikia mwisho. Nawatakia heri,” Mwangi alilia.