Joe Ageyo afurahia baada ya rais Ruto kutimiza ahadi ya kuwateua majaji 6

Ageyo alifurahia kwa sababu Ruto katika mahojiano naye alisema hiyo ndio itakuwa kazi yake ya kwanza atakapoapishwa kama rais.

Muhtasari

• Jana baada ya kuapishwa, Ruto alisema jioni hiyo atawateua majaji hao na kusimamia kuaoishwa kwao leo hii katika ikulu ya Nairobi.

Mwanahabari Joe Ageyo ni mtu mwenye furaha baada ya Ruto kutimiza ahadi alizosema katika mahojiano naye
Mwanahabari Joe Ageyo ni mtu mwenye furaha baada ya Ruto kutimiza ahadi alizosema katika mahojiano naye
Image: Facebook//William Ruto

Mtangazaji wa runinga Joe Ageyo ni mtu mwenye furaha baada ya kugundua kwamba rais mpya William Ruto amefanya kwanza kutimiza ahadi ya kuwateua majaji waliochujwa na rais Kenyatta miaka mitatu iliyopita.

 Ageyo kupitia ukurasa wake wa Twitter alidokeza kwamba wakati mmoja katika akimhoji Ruto kipindi hicho kama naibu rais na mgombea urais, alimuuliza iwapo angeteuliwa kama angewateua majaji hao waliopendekezwa na idara ya mahakama kwa rais mstaafu Kenyatta.

Ruto alimuahidi Ageyo kwamba endapo angeibuka rais, basi jambo la kwanza angefanya ni kuwateua majaji hao na kusimamia kuapishwa kwake katika ikulu siku ya pili yake kama rais.

“Katika moja ya mahojiano na DP wakati huo @WilliamsRuto. Nilimuuliza ikiwa angewateua majaji sita waliokataliwa na Rais Kenyatta, iwapo atashinda uchaguzi wa Agosti 9. Jibu lake lilikuwa na maneno matatu marefu 'Siku ya Kwanza'.” Ageyo aliandika kwa furaha kwenye Twitter yake baada ya rais Ruto kusema kwamba angewateua majaji hao hiyo jana jioni pindi tu baada ya kukamilika kwa hafla ya kuapishwa kwake.

“Ili kudhihirisha zaidi dhamira yangu ya uhuru wa Mahakama, mchana wa leo, nitawateua majaji sita ambao tayari wamependekezwa kuteuliwa katika mahakama ya rufaa, jambo ambalo lingefanyika miaka mitatu iliyopita. Kesho nitaongoza kuapishwa kwao ili waendelee na shughuli ya kuwahudumia watu wa Kenya," rais Ruto alisema Jumanne katika hotuba yake ya kwanza kama rais.

Majaji hao sita ambao wataapishwa leo hii katika ikulu ya Nairobi ni Weldon Korir, Aggrey Muchelule, Geore Odunga, Joel Ngugi ambao wote ni majaji watakaohudumu katika mahakama ya rufaa. Majaji Evans Makori na Judith Cheruyot watahudumu katika mahakama ya mazingira.