David Ndii amewataka Wakenya kumpa Ruto muda atulie ofisini

Mkiona hatuchukui simu zenu maanake tunaendelea kushughulika kulainisha mambo - Ndii.

Muhtasari

• "Ikiwa hatutachagua au kurudisha simu zako, tunashughulika,” Ndii alisema.

David Ndii amewataka wakenya kutulia na kumpa Ruto nafasi
David Ndii amewataka wakenya kutulia na kumpa Ruto nafasi
Image: Makataba

Baada ya bei ya mafuta kupanda siku mbili tu katika uongozi wa rais mpya William Ruto, Wakenya wengi wameonekana kuvunjwa moyo na tukio hilo haswa ikizingatiwa kwamba Ruto katika kampeni zake alikuwa akiwaahidi Wakenya kupunguzwa kwa bei za bidhaa kama hizo pindi atakapochukua hatamu kama rais wa 5.

Usiku wa kuamkia leo, shirika la kuratibu bei za kawi EPRA lilitangaza bei mpya ambapo mafuta ya petroli yaliongezeka kwa shilingi 20 kutoka bei ya awali ya Ksh 159 hadi Ksh 179 baada ya ruzuku iliyokuwa imeshikilia bei hizo kukamilika Septemba 14, jana.

Kupanda ghafla huko kwa bei baada ya ruzuku kutolewa kuliwachukiza Wakenya wengi ambao waligeuza suala hilo kwa njia ya kisiasa kwenye mitandao ya kijamii wakisema serikali ya Kenya Kwanza imeanza kwa dalii mbaya za kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu.

Sasa mwanauchumi David Ndii ambaye ana ukaribu sana na William Ruto na ambaye ni mmoja wa wapambaji ratiba wa UDA ameonekana kushtushwa na jinsi wakenya wamemjia juu Ruto na kupitia Twitter yake amewataka kutulia kwani kila kitu kitakuwa sawa baada ya Ruto na serikali yake kuanza kazi rasmi.

Ndii aliwataka watu kuwa wapole na kusubiria mambo mazuri hivi karibuni kwani Ruto bado ndio anaendelea kujipanga katika majukumu hayo mapya.

“Marafiki, wafuasi, wanaotakia heri. Tafadhali tafadhali tupe nafasi ya kutulia. Ikiwa hatutachagua au kurudisha simu zako, tunashughulika,” Ndii alisema.