Mwanafunzi amuua mamake katika mzozo wa kinyumbani Kisii

Mwanafunzi huyo aliripotiwa kuwa na matatizo ya kiakili

Muhtasari

• Wanafamiia walisema mzozo huo ulisababishwa na hatua ya mama huyo kujaribu kumkanya dhidi ya kuwa na ugomvi na shangazi wake mmoja, kabla yake kumgeukia kwa panga.

Crime scene
Crime scene
Image: MAKTABA

Mwanafunzi wa shule ya upili aliyemshambulia kwa upanga mama yake hadi kufa baada ya kutoroka kutoka shuleni. Baadae mwanafunzi huyo pia aliuawa na wanakijiji waliojawa na hasira mapema Jumanne asubuhi.

 

 

Clemensia Getonto mwenye umri wa miaka 76 alikuwa shambani mwake eneo la Raganga, Kitutu Chache Kusini kaunti ya Kisii mtoto huyo alipomvamia kwa oanga na kumuuwa papo hapo.

 

Wanafamiia walisema mzozo huo ulisababishwa na hatua ya mama huyo kujaribu kumkanya dhidi ya kuwa na ugomvi na shangazi wake mmoja, kabla yake kumgeukia kwa panga.

 

Kijana huyo alikuwa mtahiniwa katika shule ya St. Andrews Omogumo. Alikuwa nyumbani kwa likizo fupi ya mwezi Septemba.

 

Iliripotiwa kwamba kijana huyo amabye sasa pia ni marehemu alikuwa na historia ya matatizo ya akili na alikuwa na mazoea ya kuwaburuza wanafamilia wenzake pindi tu matatizo hayo yalipomtembelea.

 

 

Jumanne hiyo, mwanafunzi huyo alikuwa na ugomvi na shangazi yake mpaka karibu kukabana na baadae shangazi akatorokea ndani ya nyumba na kujifungia.

 

“Hapo ndio mamake aliyekuwa shambani alisikia zogo lililokuwa linaendelea na kurudi ili aweze kumtuliza mwanawe. Badala ya kutulia, alimgeukia mama yake na kummaliza papo hapo na baadaye wanakijiji walimpiga mawe na kumuua kabla atoroke,” alisema Chifu wa eneo la Raganga, Simeon Omweri.

 

Miili ya wawili  ilitolewa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kisii ili kuchunguzwa na kupanga mikakati ya mazishi.