Nairobi namba 5 Afrika kwa watu wenye utajiri mkubwa

Takwimu kutoka kwa Hazina ya Kitaifa zinaonyesha kuwa Mombasa ina watu 800 kama hao

Muhtasari

• Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Nairobi pia ina mamilionea 240 wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 10 ( shilingi bilioni 1.2)

Barabara
Image: MAKTABA

Ripoti mpya ya Henley and Partners imeorodhesha Jiji la Nairobi katika nafasi ya tano kati ya miji ya Afrika yenye mamilionea wengi zaidi. Nairobi inakuja baada ya Lagos, Cape Town, Cairo na Johannesburg.

Kulingana na ripoti hiyo, Nairobi ina Watu 5,400 binafsi wenye thamana ya juu.Wakiwa na zaidi ya dola milioni 1 (shilingi milioni 120,500,000).

Takwimu kutoka kwa Hazina ya Kitaifa zinaonyesha kuwa Mombasa ina watu 800 kama hao. Miji hiyo miwili inajivunia utajiri wa jumla wa zaidi ya dola billioni 55 ambayo ni Shilingi trilioni 6.6.

 

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Nairobi pia ina mamilionea 240 wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 10 ( shilingi bilioni 1.2)  na mamilionea 11 wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 100 (shilingi bilioni 12). 

"Haki ya kuishi, kufanya kazi, kusoma na kuwekeza katika vitovu vya utajiri vya kimataifa kama vile New York, London, Singapore, Sydney na Toronto inaweza kulindwa kupitia makazi kwa uwekezaji. Watu walio na talanta na uwezo hawapaswi kuweka maisha yao na masilahi ya biashara kwa nchi moja tu," ripoti hiyo inasema. 

Ripoti hiyo iliongeza "Kuweza kujihami, familia yako, au biashara yako hadi jiji linalofaa zaidi au kuwa na chaguo la kuchagua kati ya makazi mengi kote ulimwenguni ni kipengele muhimu zaidi cha utajiri wa kimataifa na upangaji wa urithi kwa wateja wa kibinafsi."