CJ Koome aeleza kwa nini CDF si halali

Koome alitumia fursa hiyo kufichua kwamba ni kwa sababu hiyo hiyo ambapo Mahakama ya Juu ilitangaza CDF kuwa si halali.

Muhtasari
  • Jaji Mkuu wakati huo huo alitaja ugatuzi kuwa mradi wa kikatiba ambao lazima ulindwe kwa gharama yoyote
Jaji Mkuu Martha Koome
Image: BBC

Jaji Mkuu Martha Koome amefichua sababu zilizofanya Mahakama ya Juu kuharamisha Hazina ya Maendeleo ya Eneo bunge (CDF) kuwa haramu.

Koome, akihutubia Maseneta siku ya Alhamisi mjini Naivasha, alisema kwamba hazina hiyo kitita hicho kinakiuka mgawanyiko wa majukumu kati ya serikali za kitaifa na kaunti.

CJ Koome, ambaye alikuwa mmoja wa wazungumzaji katika kikao hicho Jumatano, alitoa wito kwa maseneta kuchukua jukumu kulinda mamlaka yao ya katiba ya kusimamia vitengo vilivyogatuliwa.

Koome alitumia fursa hiyo kufichua kwamba ni kwa sababu hiyo hiyo ambapo Mahakama ya Juu ilitangaza CDF kuwa si halali.

"Hivi majuzi katika Kesi ya CDF (2022), Mahakama ya Juu ilisema kuwa ni kinyume cha sheria kugawia CDF fedha kabla ya mgawanyo wa mapato kati ya serikali ya kitaifa na ya kaunti," alisema Koome.

"Isitoshe, ilikuwa ni msimamo wa Mahakama kwamba inakiuka mgawanyiko wa majukumu kati ya serikali za kitaifa na kaunti kuruhusu CDF, chombo muhimu cha serikali ya kitaifa, kutekeleza majukumu yaliyogawiwa kwa kaunti."

Pamoja na kwamba CDF ni batili, wabunge hao sasa wanatumia Mfuko wa Taifa wa Maendeleo ya Jimbo la Serikali (NGCDF), ambao kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Yussuf Mbuno sasa watatumia fomula mpya itakayonufaisha majimbo yenye wakazi wengi na maeneo ambayo yana watu wachache.

Jaji Mkuu wakati huo huo alitaja ugatuzi kuwa mradi wa kikatiba ambao lazima ulindwe kwa gharama yoyote.