Raila Odinga amtakia Martha Karua heri njema ya kuzaliwa.

"Heri ya kuzaliwa mwandani wangu," Raila alisema.

Muhtasari

• Baadhi ya viongozi wengine pia walichukua fursa hio kumtakia Martha mema na maisha marefu.

• Mwezi wa Agosti baada ya uchaguzi mkuu, Martha alihudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mke wa mwandani wake Raila Odinga, Ida Odinga.

Mgombea urais wa Azimio One Kenya Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua katika uzinduzi wa manifesto ya Azimio 6/6/2022
Mgombea urais wa Azimio One Kenya Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua katika uzinduzi wa manifesto ya Azimio 6/6/2022
Image: RAILA/TWITTER

Aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais Raila Odinga amempongeza naibu mpeperusha bendera wake Martha Karua kwa kufikisha miaka 65 leo Alhamisi.

"Heri ya kuzaliwa mwandani wangu," Raila alisema.

Raila alimteua Karua kama mgombea mwenza katika muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kuelekea uchauzi wa Agosti 9.

Mwezi wa Agosti baada ya uchaguzi mkuu, Martha alihudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mke wa Raila Odinga, Ida Odinga.

Ida alikuwa anafikisha miaka 71.

Sherehe hiyo ilifanyika nyumbani kwake Raila na Ida kule Karen na kuhudhuriwa na wanasiasa wengineo.

Karua alizaliwa mwaka wa 1957 tarehe 22 Septemba na siku hii ameisherehekea kwa njia ya kipekee huku Wakenya wakiungana naye kumtakia heri njema ya kuzaliwa.

Baadhi ya viongozi wengine pia walichukua fursa hio kumtakia Martha mema na maisha marefu ni kama vile;

Aliyekuwa gavana wa kwanza wa Kiambu William Kabogo ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Tujibebe.

"Heri njema ya kuzaliwa mshauri mkuu wa kisheria, uishi miaka mingi," Kabogo aliandika.

"Heri njema ya kuzaliwa kwako mtu wangu naibu rais wa watu. nakutakia kila la kheri katika siku hii ya kipekee kwako," Mwanasiasa Alinur Mohamed aliandika kwenye Twitter.

Karua alifurahia kufikisha umri wa miaka 65 na alipasua mbarika hii kupitia ukurasa wake rami wa Twitter ambapo alimshukuru Mungu kwa kumwezesha kufikisha umri huo.

“Miaka 65 leo, na nazidi kumshukuru Mungu,” alisema.

Martha amewashukuru watu waliomtakia mema kwenye mitandao yake .

Martha ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amekuwa kwenye siasa kwa muda mrefu sasa. Alikuwa mbunge wa eneo bunge la Gichungu na wakili wa mahakama kuu ya Kenya.

Martha angeingia kwenye vitabu vya historia kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuhudumu katika ofisi ya naibu rais, iwapo wangeushinda uchaguzi mkuu wakiwa na Odinga.

Ni mama wa watoto wawili na na ana mjukuu mmoja ila hajaiweka ndoa yake kwenye mitandao wala kuiongelea hadharani.