Shakib Cham asherehekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake Zari

“Heri ya kuzaliwa malkia, nakupenda na nitakupenda hadi mwisho,”alisema.

Muhtasari

• Shakib alisema anajiskia mwenye baraka na mwenye bahati kumpata na kuwa naye Zari.

• Wafuasi wao mitandaoni waliububujika kumwonesha Zari upendo na kumtakia heri ya kuzaliwa.

Shakib Cham na mpenziwe Zari Hassan
Image: INSTAGRAM// SHAKIB CHAM

Mpenzi wake mwanasoshalaiti Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya amsherehekea Zari Hassan leo Ijumaa, siku yake ya kuzaliwa.

Shakib alimsifu mpenzi wake na kuzianika picha zao na Zari kisha kuandika maoni yake.

Kando na hayo Shakib alisema anajiskia mwenye baraka na mwenye bahati kumpata na kuwa naye Zari.

Aliongeza na kusema Zari ni mwanamke mwenye kushangaza kwa njia nzuri na mrembo aliyeumbika.

“Heri ya kuzaliwa malkia, nakupenda na nitakupenda hadi mwisho,” alisema.

Zari alijibu kwenye chapisho hilo na kutoa maoni yake pia na kuweka ishara ya mapenzi.

“Asante mpenzi wangu, Nakupenda sana,”alisema Zari.

Wafuasi wao mitandaoni walibubujika kumwonesha Zari upendo na kumtakia heri ya kuzaliwa.

Zari alizaliwa mwezi wa Septemba tarehe 23 mwaka wa 1980 .

Hii ni kudhihirisha kuwa Zari anahitimisha miaka 42.

Wapenzi hawa wawili wamekuwa kwenye uhusiano kwa takriban miezi mitano sasa na wamekuwa wakidokeza mikakati ya kufanya matayarisho ya harusi yao.

Jumatatu hii ,Zari alikuwa amedokeza kufunga pingu za maisha na Bw Shakib Cham baada ya kufichua kuwa mpenzi huyo wake wa sasa anapanga kupeleka posa kwa baba yake nchini Uganda.

Mama huyu wa watoto watano alibainisha kuwa mpenzi wake mpya amemletea amani ambayo imemwezesha kukua na kung'aa zaidi.

"Bwana Lutaaya chochote unachofanya, ongeza zaidi. Niongezee dozi nyingine, chochote unachofanya kwa sababu zinafanya kazi, zinafanya kazi. Hata hao wanaoroga wamekata tamaa, wanahitaji kurejeshewa pesa zao. Bado nina amani, nendeni mkaombe kurejeshewe pesa zenu," alisema Zari.

Wakosonoaji kwenye mtandao walidai kuwa Zari hupenda kuwa kwenye mahusiano na vijana wenye umri mdogo kumliko.

Zari aliwakosoa na kusema mpenzi wake Shakib si mdogo kama walivyodai.

"Mpenzi wangu sio mdogo. Ana miaka 30 anaelekea 31 Desemba mwaka huu. Yeye sio mdogo, anakaa mdogo. Mimi natimiza miaka 42 mwaka huu na huwezi kujua," Alisema.