• Duale alisema kuwa sasa mswada huo walioupitisha ndio unaowapiga mafamba vibaya mno na kuwataka kutokimbia maji ambao wameshayafulia.
Murife don’t run! Ndio habari ya mjini kwa takribani wiki mbili sasa baada ya sauti ya mwanamke fulani ikizikika kumtahadharisha mwanaume kwa jina Murife kutokimbia.
Wakenya wamekuwa wakitumia sauti hiyo kama meme ambapo wamekuwa wakiweka video za mwanaume akikimbia kwa kasi ya ajabu licha ya maneno yenyewe kumtaka Murife asikimbie.
Haya matamshi ya ucheshi sasa yamefika mpaka ndani ya majengo ya bunge. Katika kikao cha kwanza kabisa cha bunge la awamu ya 13, wabunge walikuwa wanajadili kuhusu mrengo ulioko na wingi wa wabunge kati ya Kenya Kwanza amabyo ndio umeunda serikali na Azimio la Umoja One Kenya ambao ni wapinzani.
Mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale ambaye rais Ruto alimteua kama waziri wa ulinzi, na anasubiria kuidhinishwa na bunge alisimama kutoa wasilisho lake ambapo alitumia mfano wa Murife.
Duale alisema kuwa mapema mwaka huu wakati wabunge walikuwa wanapitisha mswada wa vyama na miungano bungeni, yeye mwenyewe aliwaonya wenzake kutokimbilia kupitisha mswada huo ila wakapuuza.
Duale alisema kuwa sasa mswada huo walioupitisha ndio unaowapiga mafamba vibaya mno na kusema kuwa waliwaambia kama Murife kuwa wasikimbie lakini badala yake wakakimbia.
“Niliwaambia wabunge wakati wa Bunge la 12 kwamba Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya Siasa ingewatesa… kwa Junet na Wandayi, nasema, “Murife, Don’t run!” Duale alisema huku wabunge wakiangua kicheko.
Mjadala huo ulipamba moto ambapo hata spika mwenyewe alishindwa kutoa uamuzi wa mrengo ambao unatawala bunge kwa wingi wa viti.