"Mungu saidia" Duale amkejeli Salasya kwa kauli ya 'Madam Spika sir' bungeni

Jumatano Salasya ambaye ni mbunge wa Mumias East alikuwa anatoa wasilisho la kwanza bungeni ambapo alichanganyikiwa matamshi.

Muhtasari

• Salasya aligeuka kichekesho baada ya kumtambua naibu spikakama 'sir' ambayo ni ya kuwatambua wanaume.

Duale amkejeli Salasya
Duale amkejeli Salasya
Image: Facebook

Mbunge wa Mumias East Peter Salasya alizua gumzo na vichekesho mitandaoni Jumatano baada ya kutoa wasilisho lake bungeni kwa mara ya kwanza katika maisha yake.

Salasya ambaye ni mbunge aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa Agosti 9 alikuwa akizungumza huku akisitasita na pia kujikanganya katika kumtambua naibu spika wa bunge la kitaifa ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikao hicho.

Salasya aligeuka kichekesho baada ya kurudia makossa mara kadhaa katika wasilisho lake ambapo alikuwa anamtambua naibu spika, Gladys Shollei kama mwanaume hali ya kuwa ni mwanamke.

Wabunge na wakenya mbali mbali wamekuwa wakicheka katika video hiyo huku wengine wakimtetea kuwa ni mgeni apewe nafasi ya kuzoea na wengine wakisema kuwa alionesha mzaha katika jumba la bunge ambalo kwa muda mrefu limekuwa likihusishwa na watu walio na ufasaha katika lugha.

Mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale ambaye anasubiri kuidhinishwa kama waziri wa ulinzi alikuwa miongoni mwa wakenya ambao walizungumzia klipu hiyo ya Salasya akijikanganya kimatamshi.

Duale alisema kwa kebehi kuwa huo ni mzaha na mkanganyiko wa maneno kama huo haufai kushuhudiwa kutoka kwa mtu ambaye anawakilisha watu wake kwenye bunge la kitaifa.

“Hii ni mbaya, haiwezi kuwa katika jumba la bunge. Mungu saidia,” Aden Duale.

“Alifanya BCOM, sio elimu ingawa. Kitu pekee anachopigiwa kelele ni "Madam Spika Sir" gaffe lakini anaibua hoja muhimu na anadhihirisha kuwa atakuwa mbunge mzuri, tayari kujifunza na tayari kutetea msimamo wake,” mmoja kwa jina Michael Ollinga alimtetea Salasya.