logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gavana wa Kisii, Arati akutana na mama waliyekuwa wakiuza mboga na yeye Nairobi (+picha)

Maisha yalianzia hapa kwa mama Magi, Riruta. Hapa niliuza sukuma nikisukuma maisha - Arati alisema.

image
na Radio Jambo

Habari19 October 2022 - 05:45

Muhtasari


• Nilifurahi kurejea hapa leo; nimefurahi kuwaona tena baada ya muda mrefu!. Kicheko kizuri - Arati.

Gavana Arati akutana na wafanyibiashara wa mboga aliokuwa akishirikiana nao enzi hizo

Gavana wa Kisii Simba Arati ni miongoni mwa watu ambao walikulia katika maisha ya chini kabla ya kukwea ngazi za uongozi hadi kufika kiwango cha rais wa kaunti.

Gavana huyo ambaye bahati yake ya uongozi ilianzia jijini Nairobi wiki jana alipakia msururu wa picha akionesha kutembelea eneo ambalo alianzia maisha ya chini alipofika Nairobi kwa mara ya kwanza.

Gavana Arati akutana na wafanyikazi wadogo aliokuwa akishirikiana nao enzi za nyuma

Kwenye picha hizo, Arati alionekana akitangamana na watu kwa furaha huku akisema kwamba hapo ndio maisha yake yalipoanzia ambapo kazi yake ilikuwa kukata mboga na mama mmoja kwa jina Magi katika eneo la Riruta.

“Maisha yalianzia hapa kwa mama Magi, Riruta. Hapa niliuza sukuma nikisukuma maisha!. 😊 Nilifurahi kurejea hapa leo; nimefurahi kuwaona tena baada ya muda mrefu!. Kicheko kizuri!” Arati aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook alikopakia picha hizo.

Gavana Arati akutana na wafanyikazi wadogo aliokuwa akishirikiana nao enzi za nyuma

Arati alianza safari yake ya uongozi kama afisa wa kuhudumu katika jiji la Nairobi, almaarufu kanjo kabla ya kujaribu bahati yake katika wadhfa wa ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2013.

Alichaguliwa mbunge wa Dagoretti Kaskazini, wadhfa ambao aliushikilia kwa miaka kumi mpaka mwaka 2022 alipoamua kurudi kwao nyumbani Kisii na kuwania kama gavana.

Alikuwa mwaniaji kwa tikiti ya ODM ambapo alimbwaga mshindani wake wa karibu Ezekiel Machogu ambaye sasa ni waziri mteule katika wizara ya elimu.

Gavana Arati akutana na wafanyikazi wadogo aliokuwa akishirikiana nao enzi za nyuma
Gavana Arati akutana na wafanyikazi wadogo aliokuwa akishirikiana nao enzi za nyuma

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved