Toto asherehekea siku ya mashujaa akikata mboga kijijini

Vijana mnaopambana ili kubadilisha taswira ya mabomba yenu, nyinyi ni mashujaa - Linet Toto.

Muhtasari

• Toto aligonga vichwa vya habari baada ya kushinda uwakilishi wanawake kaunti ya Bomet akiwa na umri mchanga.

Toto asherehekea mashujaa akikata mboga kijijini
Toto asherehekea mashujaa akikata mboga kijijini
Image: Twitter

Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti ya Bomet Linet Chepkorir almaarufu Toto amewasherehekea Wakenya wapambanaji wa kipato cha kadri almaarufu mahasla kwa ujumbe maalum kama mashujaa wake.

Toto ambaye aliingia kweney vitabu vya historia kuwa mwanamke mchanga zaidi kuwahi kushinda wadhifa huo na kuwa miongoni mwa wanasiasa wachanga katika bunge la kitaifa alisema kwamba wananchi hao wanaopambana mchana na usiku kutafuta riziki wanafaa kuheshimiwa na kupewa sifa kwani bila wao uchumi wa nchi hautakua kwa njia yoyote.

Alipakia picha yake akiwa kijijini mwao huku akikata kabichi, kama kujikumbusha maisha ambayo alikuwa anapitia kabla ya kupanda ngazi katika uongozi wa kaunti ya Bomet.

“Tunapoadhimisha mashujaa mashuhuri, pia ninakumbuka vijana wa Kenya ambao wanatoka katika malezi duni lakini wanajitahidi sana na kujitolea sana kubadilisha maisha yao na taswira ya nyumba zao. Ninyi pia ni mashujaa. Heri ya Siku ya Mashujaa!” Toto aliandika kwenye picha hiyo.

Alhamisi, rais William Ruto aliongoza sherehe za mashujaa katika uwanja wa Uhuru Gardens ambapo hotuba yake ya zaidi ya dakika 20 ilijawa wingi wa mipango yake katika kuboresha uchumi wa taifa la Kenya.