logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jeridah Andayi asimulia kwa uchungu jinsi bintiye alifariki, "Nilishuhudia akifa ICU baada siku 7"

Matukio yale yalifanyika kwa haraka sana hadi tulipokuwa tukifika hospitalini, mtoto alikuwa amekufa kinadharia - Andayi.

image
na Davis Ojiambo

Habari22 October 2022 - 03:15

Muhtasari


  • • "Tukiwa njiani, ambulensi iligonga gari lingine katika mgongano wa uso kwa uso"
  • • Nilikuwa nimemshika mtoto wangu, naye akatoka mkononi mwangu, na kichwa chake kikagonga ukuta wa gari - Andayi.
Andayi aelezea jinsi alivyompoteza bintiye katika ajali huku akimkimbiza hospitalini

Mwezi wa Oktoba ni mwezi mahususi kwa kina mama waliopoteza watoto wao wachanga na unatumiwa kutoa himizo kwa kina mama hoa na kuwapa shavu kama njia moja ya kuwaliwaza.

Katika kuadhimisha mwezi huu, baadhi ya wanawake mbali mbali wamejitokeza kuzungumzia hadithi zao jinsi walivyowapoteza watoto wao wachanga, na wengine kuelezea jinsi walikishinda kipindi hicho cha majonzi makubwa – kama kila mtu atakuambia ni kwamba mama kumpoteza mtoto wake mchanga ni tukio ambalo uchungu wake hauna mfano!

Mtangazaji maarufu wa redio Jeridah Andayi ni mmoja wa wale ambao waliwahi kuwapoteza watoto wao katika umri mbichi kabisa na alizungumza na mtangazaji Cynthia Mwangi jinsi ilivyokuwa na hisia zake kumpoteza mwanawe.

Andayi aliibua kumbukumbu za majonzi jinsi mtoto wake wa miaka miwili na ushee hivi alifariki na kwa wakati mmoja alionekana kulemewa na hisia kali za huzuni.

Jeridah alisema kwamba matukio yaliyosababisha kifo cha mwanawe yalikuwa ya kutatanisha na ambayo yalitokea kwa ghafla mno kwani walikuwa katika ambulensi kuelekea hospitalini wakati gari hilo liligonga gari lingine njiani.

“Tulimuweka kwenye gari la wagonjwa ili kumkimbiza hospitali kwa ajili ya kulazwa. Tukiwa njiani, ambulensi iligonga gari lingine katika mgongano wa uso kwa uso. Nilikuwa nimemshika mtoto wangu, naye akatoka mkononi mwangu, na kichwa chake kikagonga ukuta wa gari la wagonjwa, athari hiyo ilibadilisha taswira nzima ya kila kitu,” Andayi alizungumza.

Alisema kwamba mtoto yue mgonjwa alipogongesha kichwa chake kwenye ukuta wa gari, ndio mwanzo masaibu yalianza kuongezeka na gari lile lilipojinasua kutoka ajali ile lilikwenda kwa kasi lakini walipofika hospitalini kinadharia mtoto alikuwa ameshakata Kamba.

“Matukio yale yalifanyika kwa haraka sana hadi tulipokuwa tukifika hospitalini, mtoto alikuwa amekufa kinadharia,” Andayi alikumbuka kwa uchungu.

Andayi alisema kwamba kifo rasmi cha mwanawe kilidhibitishwa baada ya siku saba akiwa kwenye sadaruki.

“Tulimweka ICU kwa siku saba na nikaona binti yangu akifa polepole. Hakupata nafuu, aliendelea kushuka na kushuka kiafya mpaka alipopumua mara ya mwisho," alisema kwa uchungu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved