Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani Imran Khan ameungana na Wapakistani na waombolezaji kote ulimwenguni kutaka wale waliohusika na kifo cha mwanahabari maarufu Arshad Sharif waadhibiwe.
Khan kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu, huku kukiwa na rundo la jumbe za rambirambi, aliomboleza Sharif kama mwanahabari mahiri na shupavu ambaye hakuwahi kuogopa kusema ukweli.
"Nilishangazwa na mauaji ya kikatili ya Arshad Sharif ambaye alilipa gharama kubwa kwa kusema ukweli - maisha yake. Ilibidi aondoke nchini na kujificha nje ya nchi lakini aliendelea kusema ukweli kwenye mitandao ya kijamii, akiwafichua wenye nguvu. Taifa zima linaomboleza kifo chake," aliandika kwenye.
Alitoa wito wa uchunguzi mkali ufanyike kuhusu mauaji hayo na kuwafikisha wahusika mahakamani.
"Uchunguzi sahihi wa kimahakama lazima uanzishwe ili kuchunguza kauli zake mwenyewe pamoja na ushahidi ambao vyanzo vingine vinao. Tumeingia katika hali ya ukatili, isiyojulikana katika jamii iliyostaarabika, iliyoingizwa na wenye nguvu dhidi ya wale wanaothubutu kukosoa na kufichua maovu," alibainisha.
Arshad Sharif's murder has sent shockwaves across Pak. It has highlighted an ongoing targeting of anyone who dares to criticise or question those holding power.When will our senior Judiciary act to ensure our citizens fundamental rights enshrined in the Constitution are protected
— Imran Khan (@ImranKhanPTI) October 24, 2022
Habari za kifo cha Sharif zilileta mshtuko kote ulimwenguni baada ya kuripotiwa kuuawa na maafisa wa polisi Jumapili usiku.