Sonko afichua sura ya mwanamume aliyejifanya mwanamke kuwalaghai wanaume wengine

Sonko aliwaambia mashabiki wake kwamba mtu huyo tayari amenaswa.

Muhtasari
  • Kutokana na jinsi mwanamume huyo alivyojipodoa,hamna mtu ambaye angemtambua kuwa ni mwanamume
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook,amefiichua sura ya mwanamume mmoja ambaye amekuwa akijifanya mwanamke.

Mwanamume huyo amekuwa akijifanya mwanamke ili kuwalaghai wanaume wenzake.

Kutokana na jinsi mwanamume huyo alivyojipodoa,hamna mtu ambaye angemtambua kuwa ni mwanamume.

Kulingana na yeye, mwanamume huyo amekuwa akiwaibia wanaume kupitia sura yake ya kupendeza kama mwanamke.

Sonko aliwaambia mashabiki wake kwamba mtu huyo tayari amenaswa.

"Imagine this cute woman is a man. Amekuwa akitoanisha wanaume pesa na kuwakunywa wakitaka kwenda na yeye anawatoshanisha ati ako na periods. Wanaume walioekwa box wakashanga kwani ni periods gani hizo haziishi kila siku. Wampangia and reported him to the police. Akawaiwa,"Sonko Aliandika.