'Unampotosha Raila,'Didmus Barasa amwambia Makau Mutua

Barasa alimwambia Mutua kwamba anampotosha Raila, na anapaswa kumuacha Raila ataafu polepole.

Muhtasari
  • Mwezi uliopita, Karua alidokeza kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Afrika Mashariki
Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa
Image: MAKTABA

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa kupitia ukrasa wake wa twitter, amemrushia vijembe msemaji wa Azimio Makau Mutua.

Hii ni baada ya Mutua siku ya Jumamosi kusema kwamba  uchaguzi wa urais nchini haujaisha.

"Hakuna anayepaswa kufikiria kuwa uchaguzi wa urais wa Kenya umekwisha. Hatujawahi kukubali chochote. Kaa chonjo," Mutua alisema.

Barasa alimwambia Mutua kwamba anampotosha Raila, na anapaswa kumuacha Raila ataafu polepole.

"Hawa watu wanaompa ushauri @RailaOdinga ndio wanampa shinikizo badala ya kumwacha Aende Retire polepole.Kenya tayari ishaa endelea rafiki zangu @makaumutua unampotosha g Raila,"Barasa Alisema.

Kauli hiyo inajiri  baada ya kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua kuwasilisha ombi katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kupinga uamuzi wa Mahakama ya upeo kuhusu uchaguzi wa urais wa 2022.

Katika marejeleo yaliyowasilishwa kortini Ijumaa, Karua na Mwanaharakati Khelif Khalifa wanateta kuwa IEBC na Mahakama ya Juu zilipuuza demokrasia na kuhujumu utawala wa sheria kupitia hatua zao katika uchaguzi wa urais wa 2022.

Mwezi uliopita, Karua alidokeza kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Afrika Mashariki.