Shirika la SOS Children Villages limezindua kampeini ya kuchangisha takriban shilingi bilioni 1.3 kwa minajili ya kuwapa misaada ya chakula na matibabu watu walioathirika na ukame katika upembe wa Afrika.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ingrid Johansen alisema mamilioni ya watu katika Upembe wa Afrika wameathirika sana na ukame wa muda mrefu.
Akihutubia makao na wanahabari Johansen alisema kuwa lengo lao hasa ni kuwasaidia watoto ambao hawana wazazi na wanahitaji sana kusaidiwa.
"Unaweza kutafakari mtoto wako kuwa bila mzazi yeyote? Au bila mtu wa kumwangalia na kumwelekeza?Ni jambo la kusikitisha," Johansena alisema.
Aliongeza kuwa wamepanga kuangazia watoto na kuhakikisha kuwa haki zao za kimsingi zinatimizwa.
Katika mikakati ya kuchangisha pesa shirika la SOS Children Villages litaandaa hafla mbali Watapanga haya kwa kuandaa shughuli za kuchangisha pesa ili waweze kutatua shida hizo katika nchi 24.
Mratibu wa majanga nchini Somalia Deqa Dimbil alisema takriban watu milioni 4 wametoroka makwao kutokana na makali ya baa la njaa.
Alisema waathiriwa wamekosa mahitaji ya kimsingi ikiwemo nyumba, chakula, mavazi na huduma za matibabu.
Kulingana na shirika la SOS Children Villages nchi zinazolengwa Kenya, Somalia, Ethiopia na miongoni mwa nchi zinginezo kanda ya Afrika Mashariki.
Shirika hilo lilisema hali ya kiangazi imesabibishwa na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu.
Nchini Kenya Shirika la SOS Children Villages linalenga kutoa misaada katika maeneo ya Turkana, Wajir, Mandera na Garissa miongoni mwa maeneo mengine.