Winnie Odinga atoa sababu ya kutaka kuwa mbunge wa EALA

Alisikitika kwamba kwa miaka mingi, nchi za Magharibi zimeingilia utawala na rasilimali za Afrika.

Muhtasari
  • Aidha alisema azma yake ya kupitishwa kuwa mwanachama wa kamati ya EALA inachochewa na matakwa yake ya kuwaunganisha vijana wa Kenya
  • Winnie alisema mfumo wa elimu nchini hauna vifaa vya kutosha kuwatayarisha kwa dunia ya sasa
Winnie Odinga
Winnie Odinga

Winnie Odinga amesema iwapo atachaguliwa katika Bunge la Afrika Mashariki, ataunda muungano wa walio tayari.

Alisikitika kwamba kwa miaka mingi, nchi za Magharibi zimeingilia utawala na rasilimali za Afrika.

Winnie alisema umoja wa wenye nia utazingatia watu na sio kusisitiza sana kwenye siasa.

Winnie alisema muungano huo utasaidia Waafrika kuondokana na uingiliaji kati wa Magharibi hadi katika bara nadhifu na lenye vifaa vya kutosha.

"Wakati mwingine ukikutana nasi utampata Mwafrika ambaye anafanya mazungumzo kama sehemu ya timu na sio wewe kuja katika nchi moja  na kuvuna na kubaka ardhi kama ulivyokuwa ukifanya," alisema.

Alisema Kenya imekuwa uwanja wa michezo kwa mataifa ya Magharibi hasa Marekani.

Aidha alisema azma yake ya kupitishwa kuwa mwanachama wa kamati ya EALA inachochewa na matakwa yake ya kuwaunganisha vijana wa Kenya.

Winnie alisema mfumo wa elimu nchini hauna vifaa vya kutosha kuwatayarisha kwa dunia ya sasa.

“Mfumo wetu wa elimu ni wa miaka 30 iliyopita, inanipa wasiwasi kwamba hata katika miaka 15, vijana wetu watakuwa wanafanya nini wakati dunia imeendelea zaidi,” alisema.