Mbunge Salasya awashukuru wakazi wa Mumias baada ya kununua V8

“Hatimaye, KDK037 imetoka na kukabidhiwa rasmi. Asanteni watu wa Mumias Mashariki kwa imani na upendo wa ajabu mlio nao kwangu.

Muhtasari
  • Alibainisha kuwa gari hilo lingemsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa wakazi wa Mumias Mashariki na Kenya kwa ugani

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salsya alizindua gari lake jipya alilonunua Toyota Land Cruiser mnamo Jumatano, Novemba 16.

Mbunge huyo katika video iliyoonekana na Radiojambo alionekana mwenye furaha huku akiwashukuru wapiga kura wake kwa fursa ya kuwa mwakilishi wao bungeni na kwa uungwaji mkono aliopewa tangu kuchaguliwa kwake.

Alibainisha kuwa gari hilo lingemsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa wakazi wa Mumias Mashariki na Kenya kwa ugani.

“Hatimaye, KDK037 imetoka na kukabidhiwa rasmi. Asanteni watu wa Mumias Mashariki kwa imani na upendo wa ajabu mlio nao kwangu.

Nitawahudumia bila kuchoka katika kutimiza ndoto zenu, na Wakenya wote kupitia kamati yangu ya kilimo, Maendeleo ya Kikanda pamoja na ushirikiano wa kikanda,” Salasya alichapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Hapo awali, mbunge huyo alikuwa akitumia gari alilokabidhiwa na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa.

Alimshukuru pia na kubainisha kuwa ataliweka wakfu gari lake jipya kwa ajili ya kuwahudumia wapiga kura wake.

 Mtindo mpya wa V8 2016 unagharimu kiasi cha Ksh10 milioni.