Mutahi Ngunyi awashauri Wakenya kumuunga mkono Winnie Odinga na Charlene Ruto

Hii inaonyesha wamejitwika jukumu la kutawala baada ya kupata uungwaji mkono wa hali ya juu kutoka kwa wananchi.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye akaunti yake ya Twitter alisema kuwa wanawake hao wawili wataenda kukuza nguvu za wasichana humu nchini

Mchanganuzi maarufu wa Kisiasa Mutahi Ngunyi amewashauri Wakenya kuwaunga mkono Winnie Odinga na Charline Ruto.

Kupitia kwenye akaunti yake ya Twitter alisema kuwa wanawake hao wawili wataenda kukuza nguvu za wasichana humu nchini.

Kulingana na taarifa yake, wanawake bado hawajafikia kile kinachofanyika Ulaya.

Aliunga mkono hilo zaidi kwa kuongeza kuwa Mawaziri Wakuu wanawake katika nchi za Ulaya hata wananyonyesha kwenye sakafu ya mabunge.

Hii inaonyesha wamejitwika jukumu la kutawala baada ya kupata uungwaji mkono wa hali ya juu kutoka kwa wananchi.

Kauli yake inajiri baada ya baadhi ya watu kukosoa uteuzi wa Winnie Odinga kwa EALA.

Aliteuliwa na muungano wa Azimio pamoja na mwanawe Kalonzo. Baadhi pia wamemtetea wakisema kuwa jina la babake halimfafanui kwa vile ana uwezo.

Kwa upande mwingine, Charlene Ruto hajateuliwa katika kiti chochote lakini hivi majuzi, amekuwa akionyesha nia ya ulimwengu wa siasa.

Ameonekana akihudhuria mikutano na viongozi hapa nchini Kenya na nje.

Ndugu wabunge Muunge mkono Winnie Odinga. Yeye ndiye maisha ya SIASA zetu na Charlene Ruto.Nguvu ya Msichana lazima Itawale. Huko Ulaya, Mawaziri Wakuu Wanawake wananyonyesha kwenye sakafu ya Bunge,"Mutahi alisema.