'Tunatazama kwa makini,'Olekina ampongeza Sankok kwa uteuzi wa EALA

Pia alidokeza kuwa, atakuwa akiangalia kwa makini kuhakikisha maslahi ya jamii yake yanawakilishwa.

Muhtasari
  • Ledama Olekina alisema kuwa marafiki wa kweli ni vigumu kupata lakini ni ukweli kwamba rais Ruto amekuwa rafiki mkubwa wa David Sankok
MBUNNGE MTEULE SANKOK
Image: RADIOJAMBO

Seneta Ledama Olekina amempongeza David Sankok kwa kuteuliwa kwake kwa bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki - EALA.

Kulingana na seneta huyo, inasikitisha kwamba chama cha ODM kilipata wanachama wote wa jamii yake hawafai kuteuliwa katika EALA.

Ledama Olekina alisema kuwa marafiki wa kweli ni vigumu kupata lakini ni ukweli kwamba rais Ruto amekuwa rafiki mkubwa wa David Sankok.

Kulingana na Seneta wa Narok, masuala ya jamii lazima yawe kipaumbele chake.

Pia alidokeza kuwa, atakuwa akiangalia kwa makini kuhakikisha maslahi ya jamii yake yanawakilishwa. 

Ni ukweli kuwa vyama vya ODM na Wiper viliamua kuwateua wanafamilia katika EALA kinyume na viongozi waliopigania uchaguzi wao vikali.

"Hongera @olesankok kama vile Shakespeare alivyosema maneno ni rahisi kama upepo,marafiki wa kweli na waaminifu ni ngumu kuwapata tunatazama kwa makini," Aliandika Olekina.

Katika muungano wa Azimio mwanawe kiongozi wa muungano huo Raila Odinga,Winnie Odinga ni miongoni mwa walioteuliwa na chama kuwa kwenye EALA.