Bobi Wine azuru Kenya afichua sababu ya ziara yake

Ameandamana na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu kutoka Uganda Kisse Besigye.

Muhtasari
  • Mwanamuziki huyo na mwanasiasa aliipongeza tume ya kitaifa ya haki za binadamu ya Kenya kwa kusimama nao
Image: BOBI WINE/TWITTER

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert almaarufu Bobi Wine yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya kikazi nchini.

Ameandamana na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu kutoka Uganda Kisse Besigye.

Wawili hao walihudhuria mkutano wa haki za binadamu wa Uganda katika sehemu isiyojulikana pamoja na wanaharakati wengine wa haki za binadamu kutoka Kenya na Uganda.

Maafisa kutoka tume ya kitaifa ya haki za binadamu ya Kenya pia walihudhuria.

Mwanamuziki huyo na mwanasiasa aliipongeza tume ya kitaifa ya haki za binadamu ya Kenya kwa kusimama nao dhidi ya utawala wa kidikteta wa rais Yoweri Kaguta Museveni.

"Tuko nchini Kenya kwenye mkutano wa haki za binadamu wa Uganda kudai haki kwa watu 100+ waliopigwa risasi na kuuawa kwa amri ya dikteta M7 wakati wa kampeni za urais kati ya tarehe 18 na 20 Nov 2020. Asante tume ya kitaifa ya haki za binadamu ya Kenya kwa kusimama nasi tuliposhinda ushindi wetu. tume yetu haiwezi" aliandika Bobi Wine.