(+video) Mwanaume apigana ngumi na polisi ndani ya kituo cha polisi

Polisi ndiye alianza kumpiga kofi mwanaume huyo kabla yake kujibu mipigo kwa kumnyanyua juu kwa juu afisa wa polisi.

Muhtasari

• Wakati wa makabiliano hayo, afisa huyo wa polisi alisikika akimuonya raia huyo kwamba hatatoka katika kituo cha polisi.

Klipu fupi ya video inayoonyesha raia akipigana mieleka na kuchapana makonde na afisa wa polisi katika kituo cha polisi mjini Nakuru imeibua mjadala kwenye mtandao.

Katika klipu hiyo ya sekunde 10, afisa huyo  wa polisi wakiwa na mwenzake wanaonekana wakiwakaribia rais waliokuwa wamesimama kwenye ukuta baada ya kuonekana kumuuliza jambo.

Jamaa huyo ambaye kama alimjibu visivyo afisa huyo alighadhabika na kufanya udhubutu wa kumzaba kofi kabla ya rais kujibu mipigo kwa kumpiga ngumi moja matata na kumnuinua hobela hibela kwa lengo la kutaka kumbwaga chini kwa kishindo.

Hali iipokuwa tete na watu waliokuwemo kituoni hapo wakishangilia, polisi wenzake waliingilia kati na kuzima fujo hiyo kwa kumnasua mwenzao kutoka mikononi mwa rais aliyekuwa na muku na lengo la kumshambulia vikali kupita maelezo.

Kulingana na taarifa zilizochapishwa na jarida la Nation, mzozo huo ulitokea katika dawati la kupiga ripoti za uhalifu kituo kikuu cha polisi cha Nakuru.

Kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Peter Mwanzo alithibitisha kisa hicho.

"Kisa hicho kilitokea katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Nakuru lakini kinachunguzwa. Nimemwomba Afisa Mkuu wa Kitengo cha Polisi (OCPD) anishirikishe maelezo ya tukio hilo ili nielewe ni nini hasa kilifanyika," Bw Mwanzo alinukuliwa na jarida hilo.

Alisema raia huyo alikamatwa na yuko chini ya ulinzi huku uchunguzi ukiendelea.

Wakati wa makabiliano hayo, afisa huyo wa polisi alisikika akimuonya raia huyo kwamba hatatoka katika kituo cha polisi.

“Hutoki ... hutoki, nakuhakikishia Hutaondoka mahali hapa, nakuhakikishia, hutaondoka”, afisa huyo anasikika akimwambia mtu huyo.

Lakini mwanamume huyo alijibu: “Nimefanya nini hadi nipigwe kofi. sijafanya lolote.”