Miguna Miguna amsuta Bobi Wine kwa kulinganisha Kenya na Uganda

Miguna alipuuzilia mbali dhana hiyo akisema Kenya ilikumbwa na vitendo haramu wakati wa uchaguzi wa Agosti 9.

Muhtasari
  • Miguna alitaja mauaji ya maafisa wa IEBC na kushambuliwa kwa makamishna wa IEBC siku ambayo matokeo ya uchaguzi yalikuwa yakitangazwa
Miguna Miguna
Miguna Miguna
Image: MAKTABA

Wakili Miguna Miguna amemsuta na kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine kwa kulinganisha Kenya na Uganda.

Bobi Wine ambaye alikuwa kwenye mahojiano katika kituo kimoja cha runinga nchini aliipongeza Kenya kwa kufanya uchaguzi wa amani hata kama alionekana kumkosoa rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kutoruhusu uchaguzi huo katika nchi jirani.

"Nilishangazwa wakati wa uchaguzi wa Kenya kwamba mtandao ulikuwa bado unaendelea, sikuona watu wakitekwa nyara au kuwepo kijeshi. Sikuona wapinzani wa aliyekuwa madarakani. chini ya kizuizi cha nyumbani," Bobi Wine alisema katika mahojiano siku ya Alhamisi.

Huku akimjibu, Miguna alipuuzilia mbali dhana hiyo akisema Kenya ilikumbwa na vitendo haramu wakati wa uchaguzi wa Agosti 9.

Miguna alitaja mauaji ya maafisa wa IEBC na kushambuliwa kwa makamishna wa IEBC siku ambayo matokeo ya uchaguzi yalikuwa yakitangazwa.

"Wakenya wasio na hatia walitekwa nyara, kutishiwa na kunyanyaswa, wakiwemo maafisa wawili wa IEBC waliouwawa. Mwenyekiti wa IEBC na makamishna wawili walishambuliwa kimwili katika Bomas of Kenya. Acha ulinganisho huu wa kipumbavu kati ya Kenya na Uganda!"