Mwanaume asimulia kubakwa na 'maid' akiwa na miaka 20

Msichana wa kufanya kazi za ndani alimtengenezea chai na mandaazi, alimsogelea na kuanza kumlisha kabla ya kumketisha juu ya meza.

Muhtasari

• Alisema kwamba siku moja akirejea nyumbani alimpata mjakazi huyo ambaye hawakuwa na mazoea ya kuzungumza naye sana ameandaa chai ya jioni na vitafunio.

• Mjakazi yule kwa weledi mkubwa alimsogelea karibu na kuanza kumlisha kabla ya kumuinua na kumketisha mezani.

Mwathirika wa ubakaji, Otieno Onyango
Mwathirika wa ubakaji, Otieno Onyango
Image: NTV Screengrab

Mwanaume mmoja kwa jina Onyango Otieno amezua gumzo kweney mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye Makala ya kipekee runingani NTV usiku wa Ijumaa akisimulia jinsi mjakazi wa nyumbani alimbaka akiwa na miaka 20.

Kulingana na Otieno, mwaka 2008 akiwa na miaka 20 mfanyikazi wa ndani nyumbani kwao alimlazimisha kushiriki tendo la ndoa naye katika kile ambacho alikieleza kuwa ulikuwa ni ubakaji.

“Mwaka 2008 nilikuwa na miaka 20, nilikuwa mwanafunzi wa kidato cha 5 katika shule moja nchini Uganda. Ilikuwa Desemba wakati wazazi wangu walimwajiri mjakazi mpya na Januari wakati kila mtu alienda shuleni na kazini, tulibaki mimi na mjakazi pekee nyumbani,” Otieno alieleza.

Alisema kwamba siku moja akirejea nyumbani alimpata mjakazi huyo ambaye hawakuwa na mazoea ya kuzungumza naye sana ameandaa chai ya jioni na vitafunio ambavyo alimpakulia ili kula.

Kilichomshangaza ni kwamba binti yule kijakazi alitaka kuketi karibu naye ii wanywe chai kwa pamoja.

“Alitaka kunisogezea kwa ukaribu kabisa mpaka kufikia kiwango cha kutaka kunilisha mandaazi. Nakumbuka akinibeba na kuniweka juu ya meza na hili sikuwahi kulisimulia kwa mtu yeyote,” Otieno alisimulia.

Baadae yule mwanadada alipata ujauzito kutokana na kitendo kile cha kulazimisha mapenzi na kijana wa watu na mamake ndiye alikuja kumpigia simu baadae akimuuliza iwapo mjakazi alimwambia ni mjamizito.

Kando na hapo, pia mamake alimwambia kwamba mjakazi yule alimwambia alikuwa na uonjwa wa zinaa. Kulingana na Otieno, hakuweza kuripoti kitendo hicho kwa mtu yeyote kwa sababu kipindi hicho hakuwa anafahamu kwamba ulikuwa ni unyanyasaji wa kingono na miaka 10 baadae aliamua kutafuta huduma za ushauri nasaha kaam njia moja ya kumponya kutokana na kitendo hicho kilichomtokea akiwa na miaka 20.