Kanini Kega:Gachagua ndiye 'kingpin' wa mlima kenya

Muhtasari
  • Gachagua ameanza kampeni kali ya kumtimua Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama kinara wa kisiasa wa Mlima Kenya
Gachagua asema Uhuru hatimaye umefika
Gachagua asema Uhuru hatimaye umefika
Image: Facebook

Mbunge mteule wa EALA Kanini Kega amesema Naibu Rais Rigathi Gachagua ndiye mfalme mpya wa Mlima Kenya.

Akizungumza siku ya Jumatano, Kanini alisema Gachagua ameweka kazi ya kuunganisha eneo hilo jambo la kupongezwa.

"Gachagua alifanya vyema katika kuunganisha eneo la Mlima Kenya. Ni kiongozi mkuu pekee tuliye naye. Tunahitaji kuungana naye kama kanda," alisema.

"Ninataka kumshukuru Gachagua ambaye aliona kuwa eneo la Mlima Kenya litakuwa na tatizo ikiwa hatutawakilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki."

Kanini pia alidai kwama alishangazwa na wabunge wa azimio ambao alidhani watampigia kura, bali waliwapigia watu asiowajua.

Aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu awali alisema Gachagua amejiweka katika njia ya kuwa mfalme wa eneo hilo kwa ‘ishara zake za mapema’ ili kulinda maslahi ya jamii.

Gachagua sasa hivi ndiye kiongozi mkuu kutoka Mlima Kenya katika serikali. Hilo linamweka mbele ya kundi,” Wambugu, ambaye alisalia mwaminifu kwa Aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta katika kampeni na uchaguzi wa 2022, alisema.

Gachagua ameanza kampeni kali ya kumtimua Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama kinara wa kisiasa wa Mlima Kenya.