Alinur azungumzia video ya mwanahabari akichapwa na walinzi wa mkewe DP Rigathi

Mara tu baada ya kumrekodi mkewwe naibu Rais Dorcas, maafisa wake wa usalama walimvamia na kumkashifu.

Muhtasari
  • Huku mwanasiasa na mfuasi sugu wa muungano wa azimio akizungumzia suala hilo alisema kwamba uhuru hatimaye umekuja kwa watu Wakenya

Mwanahabari mmoja ameripotiwa kushambuliwa kimwili na maafisa wa usalama wanaohusishwa na mkee naibu rais Dorcas Rigathi wakati wa ugawaji wa chakula cha msaada ambao aliutayarisha huko Gatanga, kaunti ya Murang'a.

Mwanahabari huyo ambaye anasemekana kuwa mwanahabari wa Daily Nation katika kaunti hiyo, aliripotiwa kuchomoa simu yake ya rununu ili kurekodi maudhui ya jukwaa la kidijitali.

Mara tu baada ya kumrekodi mkewwe naibu Rais Dorcas, maafisa wake wa usalama walimvamia na kumkashifu.

Ugomvi huo ulisuluhishwa na afisa wa polisi, kama inavyoonekana kwenye video.

Huku mwanasiasa na mfuasi sugu wa muungano wa azimio akizungumzia suala hilo alisema kwamba uhuru hatimaye umekuja kwa watu Wakenya.

Wakenya wengi waliona matamshi yake Alinur yakiwa kejeli.

"Mwanahabari kutoka Kaunti ya Murang'a kwa jina Mwangi Muiruri akipigwa na maafisa wa usalama wanaohusishwa na mke wa Naibu Rais Rigathi Gachagua, Madam Dorcas Rigathi. Haya yalijiri wakati wa hafla ya usambazaji chakula cha msaada huko Gatanga, kaunti ya Murang'a. Uhuru uko hapa watu wangu."