Ruto: Katika siku 12, tayari Ksh 1.2Bn za Huster Fund zimerudishwa na wakopaji

Katika siku 12, Hustler Fund imekopesha Ksh bilioni 7.5 kwa watumiaji milioni 15.4 kwenye jukwaa hilo - Ruto.

Muhtasari

• Zaidi ya Ksh milioni 400 zimeokolewa na Wakenya kutoka kwa Hazina hiyo - rais alisema.

Ruto aipigia debe Huster Fund
Ruto aipigia debe Huster Fund
Image: Facebook

Rais William Ruto sasa ametoa takwimu za kustaajabisha jinsi Wakenya wengi wamekuwa wakichukua mkopo wa Hustler Fund katika siku 12 tu tangu mkopo huo kuzinduliwa mnamo Desemba 1.

Rais alisema kuwa wakenya zaidi ya milioni 14 tayari waliotuma maombi ya kutaka mkopo huo wameshapewa na tayari mikopo ipatayo zaidi ya bilioni 7 imetolewa na serikali kwa wapambanaji wa chini ambao alisema wanatarajiwa kuanzisha biashara ndogo ndogo za kujikimu katika uchumi huu ambao umefumuka pakubwa.

"Katika siku 12, Hustler Fund imekopesha Ksh bilioni 7.5 kwa watumiaji milioni 15.4 kwenye jukwaa hilo," Rais William Ruto amesema.

Aidha, rais Ruto pia alisema kuwa tayari riba ya zaidi ya milioni 400 imepatikana kutokana na wale ambao wamekuwa wakirudisha mikopo hiyo, hivyo kuwatupia dongo machoni wale ambao wamekuwa wakisema kuwa mkopo wa Hustler Fund hautafaulu kwani watu wanachukua na hawawezi kurudisha – kumbe kweli watu wanarudisha eeh!

“Zaidi ya Ksh milioni 400 zimeokolewa na Wakenya kutoka kwa Hazina hiyo, zaidi ya Ksh bilioni 1.2 zimerejeshwa na wakopaji,” alisema rais.