logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto: Vijana elfu 11 wa Kazi Mtaani watapewa kazi ya kupanda miti Nairobi

Ruto alisema kuwa tayari wamefanya mazungumzo hayo na gavana Sakaja wa Nairobi.

image
na Davis Ojiambo

Habari12 December 2022 - 10:44

Muhtasari


  • • Ruto alisema kuwa tayari wamefanya mazungumzo hayo na gavana Sakaja wa Nairobi.
Rais Ruto

Kama wewe ni kijana na ambaye ulikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakifanya kazi mtaani – mradi wa kusafisha mazingira Nairobi basi nyota ya jaha imekuangazia- kama kile ambacho rais Ruto anasema ni ukweli wa kutilia maanani.

Wakati wa kusherehekea siku ya Jamhuri katika uwanja wa Nyayo Nairobi, rais katika hotuba yake alisema kuwa tayari amefanya mazungumzo na uongozi wa kaunti ya Nairobi ukiongozwa na gavana Sakaja ili kuwakimu vijana wale ambao kazi yao ilikamilika katika uongozi uliopita.

Alisema kuwa yeye na Sakaja wamekubaliana kuwapa vijana elfu 11 waliokuwa waajiriwa wa Kazi Mtaani kazi ya kurembesha mazingira ya Nairobi kwa kupanda miti na kufanya jiji kuwa la kijani – kama njia moja ya kuhakikisha lengo lake la kufikisha miti zaidi ya bilioni 15 katka miaka 10 ifikapo mwaka 2032.

“Tumekubaliana na Gavana wa Nairobi, tutaajiri vijana 11,000 ili kuunda jeshi litakaloweka rangi ya kijani kwenye jiji letu. Wale waliokuwa wakifanya kazi Kazi Mtaani,” Ruto alisema.

Ikumbukwe katika hotuba yake ya siku ya Mashujaa, Ruto alisema kuwa kazi mtaani haitokuwepo tena na vijana wote ambao walikuwa wanategemea kibarua hicho wangetafutiwa kazi nyingine, huku gavana Sakaja akisema kuwa kila mmoja ambaye alikuwa anajishughulisha katika kupanda miti basi angelipwa.

Rais amekuwa katika mstari wa mbele kuwarai Wakenya kulinda mazingira huku akiwahimiza kupanda miti kwa wingi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved