Wacha kuwapigia Wakenya kelele-Babu Owino amshauri Chebukati haya

Owino alisema kuwa Chebukati atapata kufahamu jinsi ilivyokuwa baada ya Kivuitu kugeuza matakwa ya watu.

Muhtasari
  • Kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter, Babu Owino amemshauri Chebukati kuanza kusoma historia ya Kivuitu
Babu Owino
Babu Owino
Image: Facebook

Mbunge wa Embakasi, Mhe Babu Owino amejibu kile Rais William Ruto na Wafula Chebukati wamefichua kuwa kulikuwa na njama ya kumuua Chebukati.

Babu Owino ni mmoja wa wanasiasa wakuu wa Azimio ambaye alimuunga mkono Raila Odinga kuchukua wadhifa wa rais wa tano wa Kenya.

Kulingana na Babu Owino, ametoa ushauri wenye utata kwa Chebukati kuhusu anachofaa kufanya badala ya kupiga kelele na ufichuzi wake mpya.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter, Babu Owino amemshauri Chebukati kuanza kusoma historia ya Kivuitu.

Owino alisema kuwa Chebukati atapata kufahamu jinsi ilivyokuwa baada ya Kivuitu kugeuza matakwa ya watu.

Kivuitu alikuwa mwenyekiti wa bodi ya Uchaguzi kutoka 2001 hadi 2008 ambaye alimtangaza Rais Mwai Kibaki kama mshindi katika uchaguzi wa 2007.

"Badala ya kupiga kelele/kukariri Chebukati anapaswa kuanza kusoma kuhusu historia ya Kivuitu na jinsi ilivyoisha baada ya kugeuza mapenzi ya watu. Je, Rais na Chebukati wanaweza kuacha kupiga kelele kwa Wakenya kuhusu uchaguzi uliopita.Ni maji chini ya daraja.Mheshimiwa Rais ni wakati wa kuacha kuimba na kuanza kubembea.Fanya kazi kwa Watu wa Kenya,"Babu alisema.