Kioni:Kura nyingi za Raila ziliibwa eneo la Mlima Kenya

Kutokana na maelezo yaliyotolewa, Kioni alidai kuwa na ushahidi wa udukuzi wa kura hizo na kumpendelea Rais Ruto.

Muhtasari
  • Katika utafiti huo aliousoma kwa vyombo vya habari, Kioni alisema ulifanywa na shirika ambalo linashirikiana na viongozi wanaounga mkono demokrasia barani Afrika
KATIBU MKUU WA JUBILEE JEREMIAH KIONI
Image: ANDREW KASUKU

Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni amedai kuwa kura za kiongozi wa ODM Raila Odinga ziliibwa zaidi katika eneo la Mlima Kenya.

Akizungumza alipokuwa akihutubia wanahabari jijini Nairobi, Kioni alisema udanganyifu uliofanyika wakati wa uchaguzi wa Agosti 9 ulifanyika katika eneo la Mlima Kenya.

"Udanganyifu mwingi ambao ulifanywa ulifanyika katika eneo la Mlima Kenya," alisema.

Kioni alisema kuwa taarifa zaidi zilizotolewa na shahidi zitatolewa na viongozi wa Azimio La Umoja.

"Huu ni wakati wa kusikitisha sana kwetu kama nchi. Maelezo zaidi kuhusu hatua inayofuata yatatolewa baadaye na viongozi wa muungano," alisema.

Katika utafiti huo aliousoma kwa vyombo vya habari, Kioni alisema ulifanywa na shirika ambalo linashirikiana na viongozi wanaounga mkono demokrasia barani Afrika.

Kutokana na maelezo yaliyotolewa, Kioni alidai kuwa na ushahidi wa udukuzi wa kura hizo na kumpendelea Rais Ruto.

Katika hotuba yake, Kioni alidai kuwa Raila alipata kura 8,170,355, sawa na 57.53% ya kura, na kwamba Ruto alipata kura 5,915,973, sawa na 41.66% ya kura.