"Karibu nidhani ni Chebukati!" Wanatwitter wamtania Kabogo kwa upara wake

Kwa muda mrefu , mwanasiasa huyo wa Kiambu hajawahi onekana akiwa bila kofia kichwani.

Muhtasari

• Kabogo alikuwa katika mazishi ya dadake Moses Kuria akiwa bila kofia.

• Hapo ndio wengi walipata fursa ya kuona kile ambacho amekuwa akificha kwenye kofia kwa muda mrefu.

William Kabogo ataniwa upara kama wa Chebukati
William Kabogo ataniwa upara kama wa Chebukati
Image: Twitter,

Jumatatu, aliyekuwa gavana wa kwanza wa Kiambu William Kabogo alipakia rundo la picha akiwa amehudhuria hafla ya mazishi ya dadake waziri wa biashara na viwanda Moses Kuria, Pauline Nyokabi Kuria katika kaunti hiyo ya Kiambu.

Kabogo aliungana na rais William Ruto, naibu wake Rigathi Gachagua miongoni mwa watu wengine wengi katika kumuaga dadake waziri Kuria.

“Nilijiunga na Rais H.E. Dk. @WilliamsRuto, naibu wake H.E Riggy G @rigathi na Viongozi wengine wakati wa mazishi ya Pauline Nyokabi Kuria, dada mkubwa wa Waziri wa Biashara, Uwekezaji na Viwanda Mhe. @HonMoses_Kuria katika eneo la Wamwangi katika eneo bunge la Gatundu Kusini. Mei Yeye R.i.P,” Kabogo aliandika.

Hata hivyo, gumzo kubwa halikuwa katika Kabogo kuhudhuria hafla ya mazishi, bali ni katika muonekano wake.

Kwa muda mrefu Kabogo amekuwa akionekana na kofia kichwani lakini safari hii alikuwa kichwa tupu bila kofia, jambo ambalo lilivutia maoni mengi ya utani kwenye Twitter.

Wengi walimtania kuhusu upara wake ambao ulikuwa umeangaza kweli kweli katikati ya nywele zake huku wakifananisha kichwa chake na kile cha aliyekuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, Wafula Chebukati.

Wengine walidhani kuwa hicho si kipara bali ni njia mpya ambayo mkwasi huyo wa Kiambu amekuja nayo ya kunyoa mwaka 2023.

“Kuuliza tu, hicho ni kipara ama ni staili mpya ya kunyoa mwaka mpya 2023?” mmoja kwa jina Lewis alimuuliza.

“Una hairstyle mpya, au "uwanja wa ndege" imekuwa huko wakati wote? Hutambulikani, Mhesh!” mwingine alimtania.

“Karibu nikuchanganye na Chebukati kwa hicho kichwa chako mheshimiwa,” Collins Cheruiyot alisema.