Kifungua mimba wangu ni wa baba mkwe wangu-Mwanadada amwaya mtama

Kuna wale wana uhusiano wa kimapenzi na baba mkwe, ndugu wa mume wake au mke wake, lakini wa kulaumiwa katika tabia hizi ni nani?

Muhtasari
  • Tumeshuhudia na hata kusikia jinsi ndoa za karne hii ya sasa hazidumu kama ndoa za akina babu zetu
sad woman
sad woman

Ni jambo la kusitikisha sana jinsi wanandoa wa karne hii ya sasa hawaheshimu ndoa zao au hisia za wenzi wao.

Kuna baadhi ya wanandoa ambao wanaingia katika ndoa kwa malengo tofauti na wala sio kupenda wenzi wao, au kuwa na matamanio ya kuwa kwenye ndoa.

Tumeshuhudia na hata kusikia jinsi ndoa za karne hii ya sasa hazidumu kama ndoa za akina babu zetu.

Kuna wale wana uhusiano wa kimapenzi na baba mkwe, ndugu wa mume wake au mke wake, lakini wa kulaumiwa katika tabia hizi ni nani?

Nilipokuwa kwenye ziara yangu nilipatana na mshauri wa ndoa Abednego ambaye alisisitiza kwamba hamna wa kulaumia kwa matengo haya ila sisi wenyewe.

Alitoa maoni hayo baada ya mwanamke mmoja kukiri kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba mkwe wake.

Huu hapa usimuliza wa mwanamke huyo;

"Ninapozungumzia ndoa yangu sijawahi furahi ila mume wangu aliponioa aliniacha mashambani na baba mkwe, na hapo ndipo nilianza kuwa na hisia zake,siku zilipita,miezi miaka lakini jinsi muda ulivyosonga ndipo mapenzi yetu yalivyonoga

Nahitaji ushauri  kutoka kwa Wakenya,naweza aje kumwambia mume wangu kwamba kifungua mimba wetu ni wa baba mkwe wangu yaani baba yake ,sasa imepita miaka 2 lakini ninahukumika moyoni nikimuona jinsi mume wangu anampenda mtoto wetu."

Je ni kweli kuwa nyakati za mwisho zimewadia kwani mambo kama hayo tumekuwa tukiyaona kwenye filamu,lakini yanashuhudiwa kwenye ndoa na familia zetu