logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga: Mbona ninatumia Tiktok

Niligundua kuwa kuna mwamko mpya na kuthamini Tiktok - Kahiga.

image
na Radio Jambo

Habari26 January 2023 - 05:29

Muhtasari


• "Baadhi ya wakazi wa Nyeri wameniletea masuala  mengi kwenye TikTok ambayo nyakati fulani naweza kutatua matatizo yao pale pale" - Kahiga.

Gavana wa Nyeri, Mutahi Kahiga

Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga ametetea hatua yake ya kutumia mtandao wa Tiktok ambao aghalabu huhusishwa sana na vijana wadogo.

Gavana huyo ambaye kwa zaidi ya miezi mitatu amekuwa aakionekana akishiriki video Tiktok, hadi sasa amejizolea wafuasi wapatao zaidi ya elfu 40 huku akiwa anawafuata watu elfu 10.

Mwanzoni akianzisha chaneli hiyo, gavana Kahiga alikuwa akipakia video akiimba nyimbo mbalimbali tu lakini katika siku za hivi karibuni, amekuwa akitumia mtandao huo kama njia moja ya kuwafikia wakaazi wa Nyeri na kujadili masuala ya kimaendeleo.

Japo wengi wamekuwa wakimuunga mkono kwa hatua yake hiyo, baadhi pia wamekuwa wakimtupia maneno ya kashfa lakini yeye ametoa msimamo wake kuwa anautumia mtandao huo kupata majibu ya kinachowasibu wananchi wake.

Pia alidokeza kuwa anaendelea kusomea shahada yake ya PHD na kuwa wakati mwingine akiwa amechoka akili, hujiliwaza katika mtandao huo wa kupakia video fupi fupi.

“Niligundua kuwa kuna mwamko mpya na kuthamini Tiktok. Mtu anaweza kujishughulisha mmoja mmoja na watu wengi. Tumekuwa na majadiliano ya kuelimisha juu ya TikTok moja kwa moja. Baadhi ya wakazi wa Nyeri wameniletea masuala  mengi kwenye TikTok ambayo nyakati fulani naweza kutatua matatizo yao pale pale kwa kuwashirikisha watu wengine.” alisema.

Gavana Kahiga alisema anapofika ofisini saa moja na nusu asubuhi, anarekodi video akiomba au kutoa maoni yake kuhusu matarajio ya siku hiyo na nyakati nyingine baada ya chakula cha jioni au kabla ya kulala.

"Ninasomea PhD yangu na wakati mwingine TikTok inakuwa mapumziko mazuri kutoka kwa usomaji mkubwa. Hii ni hadhira ambayo mtu anaweza kuathiri kupitia ujumbe na video ambazo mtu huchapisha... ni jukwaa la vyombo vya habari ambalo linaweza kutumika kwa njia ifaayo kuwasilisha ajenda ya mtu." alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved